WAANDISHI

HISTORIA YA SHABAAN ROBERT
Shabaan Robert (1 Januari 1909 - 22 Juni1962) alikuwa mshairi na mwandishi wariwaya. Mchango wake katika lugha yaKiswahili ni mkubwa kwani kazi zake zinaheshimika katika fasihi ya Kiswahili na pia zinatumika shuleni.

Maisha

Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 katika kijiji cha Vibambani jirani naMachuikilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga.
Wazazi wake wote wawili walikuwa wa ukoowa Mganga wa kabila la Wayao, lakini hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita Waswahili.
Hatujui sana habari za wazazi wake, lakini twajua kwamba jina la baba yake halikuwa Robert. Jina hili ama latokana na matamshi mabaya ya jina lake hasa, ama yawezekana ni jina alilopewa alipokuwa skuli Msimbazi. Inasemekana kuwa pengine alipewa naMzungu mwenye asili ya Uingereza ambaye aliitwa Robert na aliwaomba wazazi wake wamtaje jina hilo. Kwa muda mfupi yeye mwenyewe aliandika jina lake ‘Roberts’, lakini baadaye aliacha kuliandika hivyo.
Alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi,jijini Dar-es-Salaam kati ya miaka 1922 na1926, akawa mtu wa pili katika wanafunzikumi na mmoja waliofaulu mitihani yao na kupewa shahada ya kutoka chuoni, yaani School Leaving Certificate.
Akaajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karanikatika idara ya forodha huko Pangani miaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Waswahili tena mahali patulivu kulisaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.
Tangu mwaka 1944 hata 1946 alihamia ofisinyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga (tokea mwaka 1952 hata 1960).
Alipandishwa cheo kuwa Grade III Higher Division mwaka 1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena kuwa Grade II Local Service.
Kwa ujumla Shaaban Robert aliandika vitabuishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni: Adili na NduguzeKusadikikaKufikirikaWasifu wa Siti Binti SaadBaada ya Miaka Hamsini, Utubora Mkulima na Maisha Yangu.
Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha zaKichinaKiingereza na Kirusi.
Mbali na maandiko yake alikuwa na atharikubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa kamati za East Africa Swahili CommitteeEast Africa Literature Bureau na Tanganyika Languages Board. Alikuwa pia mwanachama wa Tanga Township Authority.
Alifariki dunia huko Tanga tarehe 22 Juni1962 akazikwa Machui. Aliacha wake watatuna watoto watano, ingawa aliwazaa kumi. Mke wa kwanza alikuwa Mdigo. Pia aliachadada yake (wa baba mmoja) Mwana Saumu, na mama yake.
Alitunza kwa zawadi ya waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa nishani ya M.B.E.


http://mobile.mwananchi.co.tz/makala/1604562-2770030-format-xhtml-carsoy/index.html  Au hapa
https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Shaaban_Robert

0 maoni:

Copyright © 2012 JUKWAA LA KISWAHILI - Blogger Theme by SoraTemplates