TAFSRI NA UKALIMANI

DHANA YA TAFSRI
Tafsiri imefasiliwa kuwa, ni kutoa mawazo kutoka katika lugha moja kwenda lugha nyingine bila ya kubadilisha maana. [TUKI 2002]

Mwansoko na wenzake (2006), wanafasili tafsiri kuwa ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.

Catford [1965:20] anasema tafsiri ni, “Kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja {lugha chanzi/ LC} na kuweka badala yake mawazo yanayolingana na hayo kutoka lugha nyingine {lugha lengwa/ LL}.

Mshindo (2010:2) ansema kufasiri ni kufafanua maana ya matini moja na kutayarisha baadae matini nyingine inayowiana nayo ambayo huitwa tafsiri na ambayo inawakilisha ujumbe uleule uliomo katika matini ya awali kwa kutumia lugha nyingine.

Newmark (1982) Tafsiri ni jaribio la kuwasilisha ujumbe uleule ulio andikwa katika lugha moja kwa lugha nyingine.

AS-Safi akimnukuu Dubois (1974), anaeleza kuwa tafsiri ni uelezaji katika lugha nyingine au lugha lengwa wa kile kilichoelezwa katika lugha nyingine (lugha chanzi) ikihifadhi maana na mtindo wa matini chanzi.

Nida na Taber (1969), tafsiri ni uzalisha upya ujumbe wa lugha chanzi kwa kutumia visawe asili vya lugha lengwa (LL) vinavyokaribiana zaidi na lugha chanzi, kwanza kimaana na pili kimtindo.

Larson (1984), tafsiri inahusisha uhawilishaji wa maana iliyoko katika maandishi katika lugha chanzi kwenda katika lugha lengwa. Maana zote hizo tulizoziangalia, utaona kuwa, kuna mambo matatu muhimu yanayojitokeza, mambo hayo ni:
 (i) Ujumbe/Mawazo u/ yanayotakiwa kutafsiriwa sharti yawe katika maandishi. (ii) Mawazo au ujumbe kati ya lugha chanzi na lugha lengwa sharti yalingane.
(iii) Tafsiri inaweza kuwa kutoa maana ya maneno au mawazo.
Kutokana na fasili hizo tunaweza kusema kuwa; Tafsiri ni uhawilishaji wa mawazo, ujumbe, au taarifa iliyopo katika maandishi kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa bila kupoteza maana ya msingi na mtindo uliotumika katika matini chasili.


HISTORIA NA MAENDELEO YA TAFSIRI

Wanjala (2011), anaeleza kuwa historia ni taarifa, maelezo na uchambuzi wa matukio, watu na nyakati teule zinazoathiri maisha ya wanajamii husika, sasa na hata siku za usoni. Matukio hayo huteuliwa sawia waasisi au mashujaa wa asasi hizo. Ujuzi wa historia hutuwezesha kudhibiti, na kuthamini, misingi na maendeleo ya taaaluma zetu. Kwa kurejelea ujuzi huo, pia tunaweza kubashiri mwenendo wa siku za usoni.
Ufafanuzi wa kihistoria huendelezwa kupitia vipindi bainifu vya tajiriba ya binadamu. Historia ya tafsiri imeangaliwa kwa kuegemea vipindi muhimu vya maendeleo na mabadiliko ya elimu na utamaduni. Vipindi vilivyojitenga wazi ni vitano:
👉 Enzi za kale (Old Ages)
👉 Enzi za giza (The dark Ages)
👉 Enzi za ufufuko (Renaissance period)
👉 Enzi za kati (Middle Ages)
👉 Enzi za sasa (Late Ages) p Soma historia na maendeleo ya tafsiri kwa undani zaidi hapa
Katika mada hii tutajikita kwa kuangalia kwa ufupi maana ya nadharia ya tafsiri, dhima, aina na sababu za kuanzishwa kwa nadharia ya tafsiri.
Kwa mujibu wa Mdee na wenzake (2011) wanafasili nadharia ya tafsiri kuwa ni mpango wa mawazo uliotungwa ili kueleza jinsi ya kufanya au kutekeleza jambo Fulani.
Vilevile Sengo (2009:1) anafasili nadharia kuwa ni wazo kuu, fikra kuu, mwongozo mkuu wa mtu ,watu au jamiii ya pahala Fulani kwa sababu fulani.

Kwa mujibu wa Mwansoko na wenzake (2013:7) nadharia ya tafsiri ni nguzo au muhimili wa nguzo ya tafsiri. Ni msingi wa kazi zote za tasiri. Nadharia ya tafsiri ni maeleo kuntu juu ya vipengele vinavopaswa kuzingatiwa na kila mfasiri kila akabiiwapao na kazi ya kutafsiri.

Naye Wanjala (2011:167)., anasema kuwa nadharia ya tafsiri huchunguza mbinu muafaka za kutumika katika mchakato wa kutafsiri kwa ufanisi matini ya aina Fulani mahsusi. Ni jumla ya mawazo au maarifa katika mchakato wa kufasiri; misingi na kanuni za jumla pamoja na miongozo, mapendekezo na vidokezo muhimu. Kwa kuhitimisha juu ya dhana ya nadharia ya tafsiri tunaweza sema kuwa ni mawazo au muhimili unaomuongoza mfasiri juu ya vipengele muhimu anavyopaswa kuvishughulikia katika mchakato wa kufasiri kutoka matini chanzi kwenda matini lengwa.

Newmark (1982), Mwansoko na wenzake (2006) wanasema kuna mambo matatu yaliyosababisha kuanzishwa kwa nadharia ya tafsiri ambayo ni: -
Kwanza, wingi wa makosa katika tafsiri zilizochapishwa awali. Ilionekana kwamba kulikuwa na makosa mbalimbali kama vile makosa ya kimuundo, kimaumbo, kimsamiati pia ilikuwa ni nadra kupata tafsiri zisizokuwa na makosa. Mfano: When did the rain start beating us? Tafsiri: Ni lini mvua ilianza kutupiga? Terms and condition to apply Tafsiri: Vigezo na masharti kutumika Kulingana na mifano hiyo ambayoinaonekana kuwa na makosa ya kimuundo, kimsamiati na kimaana kwa lugha zote mbili yaani lugha chanzi na lugha lengwa. Hivyo mifano hiyo ilitakiwa ionekane katika muundo ufuatao; Mfano: When did the rain start rained us? Ni lini mvua ilianza kutunyeshea? Terms and condition to be applied Vigezo na masharti kuzingatiwa Pili, kuwepo kwa idadi kubwa (na inayoongezeka) ya mashirika na asasi zinazojishughulisha na kutafsiri matini mbalimbali. Mashirika haya pamoja na watu binafsi walizua utata kwani walifasiri kwa namna tofauti matini zinazofanana. Mifano ya mashirika au taasisi hizo ni kama vile Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Tasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI), Shirika la habari la Tanzania pamoja na mashirika ya watu binafsi yanayofundisha wageni lugha ya Kiswahili. Kutoana mtafaruku huo ukazua sababu za kuzinduliwa kwa nadharia ya tafsiri ili kuweka kanuni na vigezo vinavyofanana katika kutafsiri dhana mbalimbali.
Tatu, mfumuko wa istilahi katika taaluma mbalimbali hususani sayansi na teknolojia, hivyo basi hali hii ikazua haja ya kusanifisha istilahi hizi katika lugha lengwa na chasili Mfano: Kiingereza Kiswahili
Computer -Tarakilishi
Calculator -      Kikokotozi
 Memory card  - Kadi sakima
Windows- Kiweo
Simcard -Kadiwia/ Mkamimo
 ATM- Kiotomotela
Hali hii ilihitaji nadharia ili wafasiri waongozwe na kanuni moja wanapofasiri. Hivyo nadharia ya tafsiri ilianzishwa kwa lengo la kuleta ulinganifu wa istilahi hizo kati ya lugha moja na nyingine ili kuwe na ufanisi zaidi.
Dhima za nadharia ya tafsiri ni kama zifuatavyo;
Kuonesha mbinu ambazo zinazofaa kutumiwa kufasiria aina mbalimbali za matini.
Nadharia hizi za tafsiri husaidia au humpa muongozo mfasiri kujua mbinu muhimu ambazo hazina budi kufuatwa wakati wa kutafsiri matini yoyote. Mfano wa mbinu hizo ni pamoja na tafsiri ya neno-kwa-neno, tafsiri sisisi, tafsiri ya kisemantiki na tafsiri ya kimawasiliano. Kati ya mbinu hizo mbinu ambazo hutumika zaidi ni tafsiri ya kisemantiki na tafsiri ya kimawasiliano hii ni kwa sababu mbinu hizi ndizo zinakidhi malengo makuu ya tafsiri. Malengo hayo ni kutoa taarifa na iktisadi ya lugha.
Pili, kutoa misingi, kanuni, sheria na vidokezo vya kufasiri matini na kuhakiki tafsiri, yaani matini zilizokwisha tafsiriwa. Vilevile nadharia za tafsiri humsaidia mfasiri kujua misingi, kanuni, sheria na kuhakiki matini mbalimbali za tafsiri ili kuweza kutupatia tafsiri zilizo bora. Mfano wa mambo muhimu ambayo hayana budi kuzingatiwa wakati wa mchakato wa uchambuzi wa matini ni; kwanza, kusoma matini nzima. Katika usomaji wa matini nzima dhumuni lake ni kubaini lengo la matini, kubaini lengo la mfasiri, kubaini wasomaji lengwa , umbo la matini lengwa na kubaini mtindo wa matini chanzi. Pili, kusoma matini mara ya mwisho. Pia kuna hatua (vidokezo) muhimu vya kufuata kama vile, maandalizi, uchambuzi, uhawilishaji, kusawidi rasimu ya kwanza, kudurusu rasimu ya kwanza ili kupata rasimu ya pili, kusomwa rasimu ya pili na mtu mwingine na kusawidi rasimu ya mwisho.
Tatu, kueleza jinsi ya kuvishughulikia vipengele vidogovidogo katika tafsiri kma vile maana na umuhimu wa vistari, nukta, mkato, italiki, makosa ya uchapaji na mambo mengine kwa ujumla. Kwa mfano maana na nguvu za taarifa zinazobebwa na sitiari, uwasilishaji katika matini wa maudhui na fani yote haya yana uzito sawa na mazingatio mengine ya zoezi la tafsiri. Mfano Asiyejua utu si mtu. Katika mfano huo neno utu litatiliwa mkazo katika mchakato wa tafsiri tofauti na maneno mengine yaliyo katika matini hiyo.
Nadharia mahususi za tafsiri/Aina za
nadharia ya tafsiri
Zifuatazo ni aina za nadharia ya tafsiri, tutaangalia nadharia ya usawe wa kimuundo, nadharia ya usawe wa kidhima, nadharia ya usawe wa aina-matini, na nadharia changamani.

Nadharia ya Usawe wa Kimuundo ; Nadharia hii inatetewa na mtaalam Catford (1965) Anasema kwamba, tunapofanya kazi ya kutafsiri ni muhimu kuzingatia ulinganifu wa kimuundo kati ya matini chanzi na matini lengwa hii ina maana kwamba, muundo wa matini chanzi ujitokeze katika matini lengwa. Hivyo katika nadharia hii muundo ni muhimu. Pia nadharia hii hutumika zaidi katika kutafsiri maandiko ya kidini hasa Biblia.

Nadharia ya usawe wa kidhima ;
waasisi wa nadharia hii ni pamoja na Nida (1964) na Nida na Taber (1969) wanaona kuwa usawe wa kidhima ni muhimu zaidi kuliko usawe wa kimuundo. Wanaendelea kueleza kuwa wafasiri wanapaswa kuhakikisha kwamba dhima ya matini chanzi pamoja na athari zake zinajitokeza katika matini lengwa. Yaani kama matini chanzi inawalenga watoto inapaswa iandikwe kiasi kwamba watoto wataweza kuelewa. Pia kwa kuzingatia nadharia hii unapaswa kutumia lugha rahisi na inayoeleweka na watu wote. Vilevile tafsiri yako iwe nzuri kiasi kwamba mtu atakaposoma asiweze kugundua kwamba hiyo kazi imetafsiriwa.

Nadharia ya usawe wa aina- matini ; Watetezi wa nadharia hii ni Reiss (1971), Bülher na Newmark (1982) wanasema kuwa matini yoyote ile inapaswa kufasiriwa kwa kuzingatia aina yake. Hii ina maana kwamba kazi itakayotokea (matini lengwa) ifanane na matini chanzi. Mfano kama matini chanzi ni ya kisheria itakapotafsiriwa matini lengwa nayo ionekane kuwa ya kisheria. Kinachozingatiwa katika nadharia hii ni fani (muundo) na maudhui (dhima/ lengo) ya matini yenyewe inayotafsiriwa.

Nadharia Changamani ;
 Nadharia hii iliasisiwa na P.S. Malangwa (2010) nadharia hii inadai kwamba huwezi kufanya tafsiri kwa kutumia nadharia moja tu, kwa sababu hakuna nadharia inayojitosheleza yenyewe. Hivyo basi nadharia hii ni mjumuisho au hujumuisha nadhari nyingine ili kuleta tafsiri inyojitosheleza. Hivyo nadharia ya tafsiri imechangia kuleta tafsiri bora kwani husaidia katika kuweka wazi misingi na vipengele muhimu vya kuzingatiwa katika mchakato mzima wa kutafsiri, vigezo hivi huwasaidi wafasiri kuwa na mwongozo sawa wa mambo ya kuzingatia ili kuepuka tafsiri zenye makosa.

SIFA ZA MFASIRI BORA
Mfasiri bora anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
Ø Awe mahiri wa lugha husika, hii ina maana kuwa awe anajua kwa ufasaha lugha zote mbili, yaani lugha chanzi na lugha lengwa. Hii ni kujua vizuri nyanja mbalimbali za Isimu ya lugha husika kama vile; Fonolojia- {Matamshi}, Mofolojia-{Maumbo}, Sintaksia-{Muundo} na Semantiki-{Maana}
Ø Awe na ufahamu mkamilifu wa ujumbe au mada iliyoandikwa katika matini chanzi na uwezo au jinsi ya kuelezea ujumbe au mada hiyo kwa ufasaha katika lugha lengwa.
Ø Awe mjuzi wa TEHAMA
 Ø Ajue lugha mbili au zaidi.
 Ø Awe na tajiriba kubwa ya usomaji wa aina mbalimbali za tafsiri na kujiendeleza kulingana na mabadiliko ya kijamii.
 Ø Afahamu vizuri watu, jamii na utamaduni wa watumiaji wa lugha chanzi na lugha lengwa.
Ø Afahamiane na watu wengi, yaani kujichanganya changanya na watu wa fani au sekta mbalimbali.
Ø Awe na tabia yakushirikiana na watu wengine katika shughuli za kufasiri.
i. Uaminifu, mfasiri bora anapaswa kuwa mwaminifu moja kwa moja kwa mteja wake na matini anayoitafsiri.
ii. Anayejituma na kufanya kazi kwa bidi iii. Anapaswa kuelewa na kuzingatia tartibu za kazi zake. Mfano makubaliano na mteja yawe kwa mkataba wa maandisi ambao utataja mteja ni nani au taasisi, mfasiri, aina ya kazi, lugha asilia, idadi ya kurasa, taratibu za malipo pamoja na kiwango pia kazi hiyo itakamilika baada ya muda gani.  iv Mfasili bora ni yule ambaye ana ushirikiano na wafasili wenzake na watu wa sekta nyingine.
 v. Aepuke vishawishi, yaani asiwe na tamaa awe na msimamo. {asijipendekeze wala kujishusha kwa mteja}
 i. Awe nadhifu, yaani nadhifu wa moyo na muonekano.
Tafsiri ina dhima zifuatazo:
§ Ni njia ya mawasiliano
 § Nyenzo ya kueneza utamaduni kutoka jamii moja hadi nyingine.
 § Mbinu ya kujifunza lugha za kigeni.
§ Mbinu ya kukuza lugha.
 § Ni kiliwazo cha mfasiri.
 § Njia ya kuongeza kipato.{Kiuchumi}

Mawasiliano ni nguzo kuu ya uhai, maelewano na maendeleo ya jamii. Mawasiliano ni njia inayofanya kazi kama daraja kati ya watu au jamii mbili zinazotumia lugha tofauti. Mfano maelekezo ya insi ya kutumia bidhaa kama vile dawa, simu redio n.k, pia mikataba ya kimataifa hutafsiriwa katika lugha mbalimbali kutegemeana na jamii husika. Karibu mataifa yote yanatambua umuhimu wa jamii ya kimataifa. Nayo jamii ya kimataifa imeafikiana maazimio mengi kuhusu tabia, hali na mienendo ya watu, kama vile haki za kibinadamu, haki za watoto na umuhimu wa mazingara ya ulimwengu. Maazimio haya yametafsiriwa kwa lugha zinazozungumzwa kwa wingi ili kufikia watu wengi iwezekanavyo. Watawala wa mataifa binafsi nao wanahakikisha kuwa taarifa muhimu kwa jamii yote zimetafsiri kwa lugha inayoeleweka na raia wengi, ili waweze kujisomea au kusomewa na wenzao. Humu nchini makala nyingi ambazo hapo awali zilikuwa zimeandikwa kwa Kiingereza zimefatafsiriwa au kufanyiwa mpango wa kutafsiriwa kwa Kiswahili.
Utamaduni unahusu maswala mengi ya maisha ya jamii. Hapa tutafikiria zaidi falsafa za maisha, zinavyoenezwa kupitia matumizi ya lugha na fasihi. Ngano na tanzu zingine za fasihi ni hifadhi za tamaduni za lugha zake. Tunapotafsiri fasihi, tunafuma baadhi ya vipengele vya utamaduni wa lugha chasili kwa utamaduni wa lugha pokezi. Mafunzo yanayopatikana katika tafsiri za lugha zingine za Kiafrika -fasihi simulizi– sasa ni amali ya Kiswahili. Tafsiri za Kiarabu, Kiingereza na lugha zingine pia zimechangia ujenzi wa lugha ya Kiswahili. Tunapotafsiri pia tunajenga lugha pokezi: lugha pokezi inamotishwa kukua na wakati wake na kumiliki nyenzo za kuhimili miradi ya kijamii. Mfano
Dini ni nguzo muhimu inayohimili jamii nyingi. Katika kusambaza utamaduni na Imani za Kikristo, wamishenari walitafsiri Biblia na mafunzo mengine kwa lugha nyingi kote ulimwenguni. Vilevile, Waislami walitumia mbinu kama hiyo na kutafsiri Korani na mafunzo kama Hadithi kwa lugha nyingi. Ni jambo rahisi zaidi kufikia roho ya mtu kwa lugha yake kuliko ile ya wageni. Bila tafsiri, dini nyingi hazingesambaa kadiri zimekuja kufanikiwa. Kumbuka, dini hizi zilisambaa sawia elimu ya mwegemeo wake. Mbinu ya kujifunza lugha za kigeni, mfasiri anapofanya kazi ya kutafsiri hukumbana na changamoto mbalimbali na anapohitaji kuzitatua changamoto hizo hujifunza lugha katika kipengele cha msamiati, sarufi, maana na nyongeza au maana za kimuktadha.
Kuainisha matini ni kuzigawa au kuziweka matini katika makundi mbalimbali kwa kuzingatia kufanana kwake kwa sifa kadhaa. Sababu za kuainisha matini za tafsiri, Ili kupata aina au makundi kadhaa yatakayotuongoza kuchagua njia au mbinu ya kutafsiri. Hii ni kwa sababu kila aina fulani ya matini hutafsiriwa vizuri zaidi kwa kutumia njia au mbinu fulani.

Mikabala /vigezo vya uainishaji wa matini za tafsiri
 a) Kigezo cha mada
b) Matumizi ya istilahi
c) Dhima kuu za lugha

Katika kigezo hiki kinachoangaliwa ni kwamba matini inaongelea nini au inahusu nini kwa mtazamo wa kijumla. Kwa kutumia kigezo hiki cha mada tunapata aina tatu za matini;
i. Matini za kifasihi. Ni matini zinazohusu maandiko ya kifasihi kama hadithi fupi, riwaya, tamthiliya, ushairi n.k.
 ii. Matini za kiasasi. Ni matini zinazohusu siasa, biashara, fedha, sheria, serikali na asasi nyinginezo. Mfano wa Matini hizi za kimamlaka ni kama vile matini za kisiasa na kiserikali (hotuba, risala, mikataba, vyeti nk).
i. Matini za kisayansi.
Ni matini zinazojumuisha nyanja zote za sayansi na teknolojia. Mfano maelekezo ya matumizi ya vifaa mbalimbali vya kielektroniki
Kigezo hiki huangalia kiwango cha matumizi ya istilahi za uwanja fulani hivyo matini huainishwa kwa kuangalia wingi au idadi za istilahi au msamiati maalumu kwa ajili ya taaluma husika. Hivyo kwa kuangalia idadi ya istilahi tunapata aina tatu za tafsiri ambazo ni;
 i. Kiufundi
 ii. Nusu- ufundi
iii. Matini zisizo za kiufundi (matini za kawaida)
i) Matini za kiufundi (Technical text), hizi huwa na idadi/matumizi makubwa ya istilahi.
ii) Matini za nusu ufundi (Semi- Techinical Text), huwa na kiwango cha kati cha matumizi ya istilahi (zinakuwa na istilahi chache).
iii) Matini zisizo za kiufundi (Non- technical text), hizi zinakuwa hazina matumizi ya istilahi na hivyo hutumia msamiati wa kawaida
Kwa kutumia kigezo hiki matini za tafsiri huainishwa kwa kufuata aina za dhima kuu za lugha zilizopendekezwa na Bülher (1965) ambazo ni;
 I) Dhima elezi (Expressive function); Ni aina ya matini ambayo hujiegemeza zaidi kwa mwandishi, mwandishi anatumia lugha kuelezea hisia zake bila kujali ujumbe huo utapokelewa vipi na wasomaji. Mfano mzuri wa matini elezi ni kazi mbalimbali za fasihi kama vile: ushairi, hadithi fupi, tamthiliya, riwaya, hotuba, nyaraka za kisheria, wasifu nafsi, insha nk.

II)Dhima arifu (Informative function) Hapa lugha hutumika kutolea taarifa. Kiini cha dhima hii ni ukweli wa mambo/taarifa yenyewe. Matini hizi huwa zinaandikwa katika maumbo sanifu, mfano vitabu, ripoti za kiufundi, tasnifu au Makala katika magazeti ama majarida ya kitaaluma n.k )

III) Dhima amili (Persuasive function) Ni aina ya matini ambayo imeegemea zaidi upande wa wasomaji. Matini amili zinalenga kuibua hisia za msomaji na kumfanya afikiri au atende kwa maana ambavyo imekusudiwa na matini mahususi. Hivyo lugha hutumika kuchochea hisia za msomaji na kiini cha dhima hii ni hadhira. Mfano wa matini hizi ni matangazo, maombi mathalani ya kazi au kitu kingine, maelekezo, propaganda na mialiko.
Kwa kuzingatia dhima hizo tatu za lugha kwa mujibu wa Bülher (1965) tunapata aina tatu za matini ambazo ni;

 i) Matini Elezi Matini hizi huegemea zaidi upande wa mwandishi, mfano fasihi, maandiko ya kimamlaka kama vile hotuba, mikataba, maandiko ya kisheria, maandiko ya kitaaluma, wasifu, tawasifu, shajara, wosia n.k.
ii) Matini arifu Matini ambazo hulenga kutoa taarifa na hata maarifa kuhusu jambo fulani kama vile vitabu vya masomo/taaluma mbalimbali. Matini arifu huwa na muundo maalumu Mfano; umbo la jarida, makala, ripoti, tasnifu, vitabu vya taaluma mbalimbali n.k.
iii) Matini amili Matini amili huegemea zaidi upande wa hadhira, Katika matini Amili mwandishi hujitahidi kadiri awezavyo kuchochea hisia za wasomaji na kuwafanya watende kama ambavyo anavyotaka watende/ wafanye. Mfano wa matini hizo ni kama vile mialiko (barua na kadi, matangazo, maelekezo (jinsi ya kutumia kitu) n.k.
Kuchambua matini maana yake ni kuisoma matini husika kwa kina na kuielewa kabla ya kuanza kuifasiri/kuitafsiri. Pia sababu au umuhimu wa kuchambua matini za tafsiri ni ili kubaini sifa na vipengele vinavyojenga matini husika kifani, kimaudhui na hata kiitikadi.
Kuna vipengele vikuu vitatu, ambapo kila kipengele kina hatua kadhaa ndogondogo. i. Kusoma matini nzima/ yote. Faida ya hatua hii ni kwamba humsaidia mfasiri kuweza kuandaa marejeleo muafaka, kuandaa vitabu au machapisho mbalimbali (kama vile kamusi ya lugha moja au mbili) yatayomsaidia katika zoezi zima la kufasiri matini. Pia hatua hii itamsaidia mfasiri kuandaa orodha ya istilahi na visawe vitakavyohitajika katika suala zima la tafsiri. Vilevile itamwezesha mfasiri kugawa vipengele/sehemu miongoni mwa wafasili hasa kama matini ni kubwa.

ii. Kuchambua matini yenyewe. Uchambuzi wa matini hulenga kupata nduni/sifa bainifu za matini husika. Kipengele hiki kina hatua tano kama ifuatavyo;

a) Kubaini lengo la mwandishi wa matini chanzi. Mfano; malengo ya mwandishi huweza kuwa kukweza, kubeza kusifu, kukashfu au kuarifu jambo.
Hivyo katika uandishi mwandishi anaweza kuwa na mtazamo mmoja kati ya hii mitatu;
Ø Mtazamo h a s i k w a mtendwa
Ø Mtazamo c h a n y a k w a mtendwa
 Ø Mtazamo w a k a ti .

 b) Kubaini lengo la mfasiri (mteja). Mfasiri hapa inabidi ajiulize kwa nini anataka kutafsiri matini husika. Pia mfasiri ajiulize kwa nini mteja wake anataka matini hiyo itafsiriwe. Hivyo mfasiri anapaswa kuepuka upendeleo au kuegemea upande mmoja badala yake anapaswa kuwa na msimamo wa katikati hata hivyo ni muhimu sana kwa mfasiri kuzingatia hadhira lengwa.

c) Kubaini hadhira na umbo la matini. Hapa mfasiri atajiuliza maswali kama vile: - hiyo matini anayofasiri ni aina gani ya matini? je aina hiyo ya matini inatafsirika vizuri zaidi kwa kutumia njia/mbinu gani? Je hadira lengwa ya zao la tafsiri ni ipi na ina sifa gani? Mfano hadhira wana elimu hadi ngazi ipi, umri wao, mahali wanapoishi n.k. Pia zao la tafsiri linapaswa kuwa katika umbo gani?

 d) Kubaini mtindo wa matini. Ni muhimu sana mtindo wa matini chanzi kujitokeza katika matini lengwa. Mfano kama matini chanzi ipo kwenye mtindo wa monolojia, dailojia, hadithi, lugha za mitaani au mtindo wa kidini hivyohivyo matini lengwa inatakiwa kuwa katika mtindo wa matini chanzi.
 e) Kubaini ubora na mamlaka ya matini. Ubora wa matini chanzi hutokana na kuzingatia zana za kiisimu. Hivyo mfasiri hanabudi kuzingatia ujuzi wa mwandishi katika kutumia zana za kiisimu (vipengele mbalimbali vya lugha).
 Kwa upande wa mamlaka ya matini chanzi hutokana na hadhi/ubobevu wa mwandishi katika taaluma husika.

 ii. Kusoma matini kwa mara ya mwisho. Mfasiri katika hatua hii inabidi asome tena matini chanzi ili kutoa taswira au kuwekea alama maneno au maumbo muhimu katika matini. Baadhi ya maneno au mambo huhimu ya kuzingatia ni kama vile majina mahsusi ya watu, sehemu, takwimu na pia miaka. Vilevile kuna maneno ambayo hayatafsiriki kirahisi hivyo itambidi mfasiri ayawekee alama ili iwe rahisi kwake katika kutafuta visawe.
Baadhi ya wataalamu wanasema kuna hatua 5 wengine 6,7 na wengine wanadai zipo hatua 8. Hapa tutachambua hatua 6 kama zinavyopendekezwa na Mwansoko na wenzake 2006.

Hatua hizo zilizoainishwa na Mwansoko na wenzake 2006 ni zifuatazo;
 i. Maandalizi
 ii. Uhawilishaji
iii. Kusawidi rasimu ya kwanza ya tafsiri (drafting)
iv. Kudurusu wa rasimu ya kwanza ili kupata rasimu ya pili ya tafsiri v. Kusomwa kwa rasimu ya pili na mtu mwingine
vi. Kusawidi wa rasimu ya mwisho ya tafsiri
Hatua hii inahusisha mambo matatu ambayo ni:
 a) Kupitia tena sehemu muhimu za matini chanzi, kwa mfano; istilahi, majina ya wahusika, majina ya kijiografia, maeneo au kauli zisizofasirika kirahisi.
b) Kupata marejeleo ili kutafuta visawe vya kisemantiki kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa.
 c) Kutafuta na kuandika maneno au visawe hivyo.

Hivyo katika hatua hii, mfasiri anatakiwa kufahamu vizuri maudhui ya matini chanzi, ujumbe wake, mtindo wa matini na kuwekea alama sehemu zenye utata au zisizoeleweka vizuri, anashauriwa kupigia mstari au kuandika katika kidaftari kidogo msamiati, istilahi na misemo muhimu ya matini chanzi kama vile, methali, nahau maneno ya kitamaduni yasiyotafsirika, majina maalumu, n.k. kwa kupigia mstari au kuyaandika katika kidaftari kidogo ili iwe rahisi kwa mfasiri kuyatafutia visawe vyake kabla hata ya kuanza kutafsiri lakini pia kumsaidia mfasiri asiyasahau wakati wa kutafsiri au kuyatolea ufafanuzi zaidi katika tafsiri yake.
Uahawilishaji maana yake ni kuhamisha ujumbe, maana n.k kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa kwa kuzingatia sarufi ya lugha lengwa, lengo, mawazo, umbo la matini, mtindo wa matini n.k. Hii ina maana kuwa katika hatua hii, visawe vya kisemantiki [kimaana] vya matini chanzi vilivyobainishwa katika hatua ya awali (maandalizi) huamishwa katika matini lengwa [kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa] na kupangwa vizuri kisarufi na kimantiki ili fasiri hiyo iwe na maana kwa wasomaji wake.
Uhawilishaji wa visawe kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa unapokamilika kinachopatikana ni rasimu ya kwanza ya tafsiri. Katika hatua hii, mfasiri huandika rasimu yake ya kwanza ili kupata picha fulani ya matini aliyoikusudia, katika uandaaji wa rasimu ya kwanza, kwa kufanya hivi, mfasiri anaweza kugundua kuwa anahitaji taarifa zaidi tofauti na alizozipata katika hatua ya awali, na hivyo kulazimika kuchunguza zaidi matini chanzi na hata kupekua zaidi na zaidi marejeo yake aliyoyaandaa kwa kuyatumia katika tafsiri. Jambo la kuzingatia, mfasiri anatakiwa wakati akihamisha mawazo au ujumbe azingatie umbo na lengo la matini chanzi ili kutoathiri tafsiri yake. Hivyo rasimu ya kwanza ya tafsiri inakuwa na dosari nyingi na kwa hiyo haifai kupelekwa kwa mteja au hadhira. Badala yake rasimu ya kwanza lazima ipitiwe tena upya na kurekebishwa au kudurusiwa/ durusu (review) rasimu (draft).
Baada ya kusawidi rasimu ya kwanza, mfasiri anatakiwa kuivundika rasimu yake ya tafsiri, Larson (1984) anashauri kuwa rasimu ya kwanza iachwe kwa muda kidogo kati ya juma moja hadi mawili tangu kukamilika kwake na kuanza kuidurusu/ kuipitia rasimu hiyo kwa jicho la kihakiki zaidi na kuangalia kama kuna makosa ambayo yamejitokeza katika rasimu yake au la na kuyafanyia marekebisho pale inapobidi. Mfasiri katika hatua hii anatakiwa kuisoma rasimu yote ya tafsiri (kwa sauti) ili aweze kufanya mambo yafuatayo;
 ð Kunyoosha sehemu zenye tafsiri ya mzunguko na zenye matumizi potofu ya visawe.
 ð Kurekebisha sehemu zenye miunganiko tenge inayozuia mtiririko mzuri wa matini. ð Kuhakiki usahihi na ukubalifu wa maana zilizowasilishwa katika matini lengwa.
 ð Kuhakiki ukubalifu wa lugha iliyotumika katika matini lengwa kulingana na umbo la matini ya lugha chanzi.
 ð Kuona iwapo mada au ujumbe mkuu wa matini chanzi unajitokeza waziwazi katika matini lengwa.

Matokeo ya kudurusu rasimu ya kwanza huwa ni kupatikana kwa rasimu ya pili. Ingawa rasimu ya pili inakuwa bora zaidi kuliko rasimu ya kwanza bado kuna haja ya ya rasimu ya pili kusomwa na mtu mwingine tofauti na mfasiri mwenyewe. Hii ni kwa sababu mtu wa pili anaweza kung’amua dosari ambazo mfasiri hakuziona. Msomaji wa pili anaweza kuwa mfasiri, shabiki wa tafsiri, mhakiki wa tafsiri, mhariri, mteja wako au mtu mwingine unayemwamini.
Pia wakati mwingine msomaji wa pili hatakiwi kujua kwamba anachosoma ni tafsiri hivyo mfasiri anaweza kumficha. Hivyo ni vizuri zaidi msomaji wa pili kusoma kwa sauti ili aone ni wapi hapana mtiririko mzuri (yaani wapi anakwamakwama) ili aweke alama ambapo anakwama ili kumsaidia mfasiri wakati wa kurekebisha.
Katika hatua hii mfasiri atafanyia kazi maoni ya msomaji wa pili, mfasiri anaweza kuyatumia maoni, mapendekezo na maelekezo ya msomaji wa pili akiona yanafaa ili kuweza kusahihisha tafsiri yake na hatimaye kuandaa na kutoa rasimu ya mwisho ambayo kwa hakika ndiyo tafsiri yenyewe iliyokamilika. Rasimu hii ya mwisho ndiyo hupelekwa kwa mteja, hadhira, au wachapaji (kuchapisha kuwa kitabu) iwapo hilo ndilo lengo

DHANA YA UKALIMANI

Kwa mujibu wa KADE (1968) anafasili ukalimani kuwa ni aina fulani ya tafsiri ambapo matinichanzi huwasilishwa mara moja pekee na hivyo haiwezi kupitiwa upya, kuchezwa upya au kurudiwa pia matini lengwa hutolewa katika muda finyu huku kukiwa hakuna fursa ya marudio au masahihisho na kama fursa hiyo ipo basi ni finyu sana.

 Naye Pӧchhacker (2004) aliboresha fasili iliyotolewa na KADE (1968) na kuja na fasili ifuatayo ya ukalimani, anasema ukalimani ni aina fulani ya tafsiri ambapo matini lengwa hutolewa mara moja tu katika muda finyu na kwa ajili ya matumizi ya muda wa wakati huohuo.

Hivyo basi kwa kuangalia fasili hizo mbili tunaweza baini kuwa msingi wa ukalimani ni hali ya papo kwa papo ya uwasilishaji. Kwa jumla, ukalimani ni uhawilishaji wa ujumbe au maudhui yaliyo katika matini chanzi kwenda katika lugha lengwa ambapo mkalimani hubanwa na muda na hivyo kukosa fursa ya kurudia kusikia matini chanzi wala kuihawilisha lakini pia uhawilishaji hulenga kuinufaisha hadhira lengwa papo hapo.

a) Awe na ujuzi wa hali ya juu wa lugha anazoshughulika nazo pamoja na utamaduni wake.
b) Ajue lugha zaidi ya mbili za kimataifa kwani kadiri unavyojua lugha zaidi ndivyo unavyokuwa mkalimani bora zaidi. Pia lugha zaidi ya moja hasa za kimataifa zitamsaidia sana hasa kwenye mikutano/ makongamano.
 c) Awe na ujuzi au maarifa ya kutosha juu ya mada, taaluma au uwanja unaozungumziwa. Inamaana kwamba kama wewe ni mkalimani wa masuala ya kiuchumi basi hupaswi kufasili masuala ya kisheria. Mfano; ukalimani wa mahakamani hufanywa na wanasheria, masuala ya tiba n.k
d) Awe na ujuzi wa taaluma ya ukalimani; yaani awe amepata mafunzo ya ukalimani. Katika hayo mafunzo atajifunza mbinu za ukalimani aina, changamoto na namna ya kuzikabili changamoto hizo.
e) Awe na kipaji, yaani; Yaani uwezo wa kukumbuka kwa hali ya juu, Kuteua msamiati sahihi kwa haraka, Kipaji katika kuunda istilahi haraka haraka na kuitumia. Kipaji cha ulumbi/ awe na ulumbi yaani kipaji cha kuongea na kuvuta/kushawishi watu.
f) Awe mchapakazi, mdadisi na nayependa kujiendeleza na kupata habari kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii mfano; magazeti, majarida, televisheni, facebook, twitter au kuzungumza na watu/ kuchangamana na watu.

CHANZO: https://antagonf.blogspot.co.ke/2014/10/tafsiri-na-ukalimani.html?m=1

8 maoni:

UKALIMANI NA TAFSRI

Ikiwa wahitaji kujua kutafsri na kukalimani vizuri pakua kitabu hiki cha Bure kabisa,,hautojilaumu.https://antagonf.blogspot.co.ke/2014/10/tafsiri-na-ukalimani.html?m=1

0 maoni:

METHALI 610 ZA KISWAHILI
-------------------------------------------

1. Aanguaye huanguliwa.
2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu.
3. Abebwaye hujikaza.
4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti.
5. Adui aangukapo, mnyanyue.
6. Adui mpende.
7. Adui wa mtu ni mtu.
8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna.
9. Ahadi ni deni.
10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
11. Akiba haiozi.
12. Akili ni mali.
13. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
14. Akili nyingi huondowa maarifa.
15. Akutukanae hakuchagulii tusi.
16. Akipenda chongo huita kengeza.
17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki.
18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema.
19. Akupaye kisogo si mwenzio.
20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
21. Alisifuye jua, limeuangaza.
22. Aliye juu msubiri chini.
23. Aliye kando, haangukiwi na mti.
24. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi.
25. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua.
26. Akufukuzae hakwambii toka.
27. Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa.
28. Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga.
29. Ana hasira za mkizi.
30. Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga.
31. Angurumapo simba, mcheza ni nani?
32. Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi.
33. Apewaye ndiye aongezwaye.
34. Anaejipiga mwenyewe, halii.
35. Asifuye mvuwa imemnyea.
36. Asiye kubali kushindwa si mshindani.
37. Asiye kujua, hakuthamini.
38. Asiye kuwapo na lake halipo.
39. Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu.
40. Asiye na mengi, ana machache.
41. Asiye uliza, hanalo ajifunzalo.
42. Asiyejua maana, haambiwi maana.
43. Atangaye na jua hujuwa.
44. Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali).
45. Atekaye maji mtoni hatukani mamba.
46. Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
47. Baada ya dhiki faraja.
48. Bahari hailindwi.
49. Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume.
50. Bandu bandu huisha gogo.
51. Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
52. Bendera hufuata upepo.
53. Biashara asubuhi.
54. Bilisi wa mtu ni mtu.
55. Bora kinga kuliko tiba.
56. Bora lawama kuliko fedheha.
57. Bora mchawi kuliko fitina.
58. Biashara asubuhi.
59. Bora nusu shari kuliko shari kamili.
60. Bwawa limeingia ruba.
61. Cha mtu mavi.
62. Chaka la samba, halilali nguruwe.
63. Chamlevi huliwa na mgema.
64. Chanda chema huvikwa pete.
65. Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako.
66. Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza.
67. Chombo cha kuzama hakina usukani.
68. Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
69. Chui hakumbatiwi.
70. Chururu si ndo ndo ndo.
71. Dalili ya mvua mawingu.
72. Damu nzito kuliko maji.
73. Daraja livuke ulifikapo.
74. Dawa ya moto ni moto.
75. Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea.
76. Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
77. Dawa ya moto ni moto.
78. Donda ndugu halina dawa.
79. Dua ya kuku haimpati mwewe.
80. Fadhila huna, hata hisani hukumbuki?
81. Fadhila ya nyuki ni moto.
82. Fadhila ya punda ni mateke (mashuz)
83. Fahari ya macho haifilisi duka.
84. Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
85. Fata nyuki ule asali.
86. Fimbo ya mbali haiui nyoka.
87. Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua.
88. Funika kombe mwanakharamu apite.
89. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
90. Gome la udi, si la mnuka uvundo.
91. Haba na haba, hujaza kibaba.
92. Haki ya mtu hailiki.
93. Hakuna masika yaso mbu.
94. Hakuna msiba usio na mwenziwe.
95. Hakuna siri ya watu wawili.
96. Hakuna ziada mbovu.
97. Hala hala mti na macho.
98. Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi.
99. Hapana marefu yasio na mwisho.
100. Haraka haraka haina baraka.
101. haraka haraka haina baraka.
102. Haramu yako halali kwa mwenzio.
103. Hasidi hasada.
104. Hasidi mbaya.
105. Hasira, hasara.
106. Hatua ndefu hufupisha mwendo.
107. Hauchi hauchi, unakucha.
108. Hayawi hayawi, mara huwa.
109. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
110. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
111. Heri nitakula na nini?, kuliko nitakula nini?
112. Heri ya marama kuliko kuzama.
113. Hiari ya shinda utumwa.
114. Hogo halihogoki mpaka kwa hogo jenziwe.
115. Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
116. Ila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda.
117. Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo.
118. Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo.
119. Imara ya jembe kaingojee shambani.
120. Jambo usilolijua, usiku wa giza.
121. Jina jema hungara gizani.
122. Jini likujualo halikuli likakwisha.
123. Jino la pembe si dawa ya pengo.
124. Jitihada haiondoi kudura.
125. Jitihadi haiondoi kudura.
126. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
127. Jungu kuu, halikosi ukoko.
128. Jununu fununu.
129. Kafiri akufaaye, si muislamu asiye kufaa
130. Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
131. Kama hujui kufa,tazama kaburi.
132. Kama wewe wasema cha nini, mwezio asema nitakipata lini.
133. Kamba hukatika pabovu.
134. Kanga hazai ugenini.
135. Kawaida ni kama sheria.
136. Kawia ufike.
137. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
138. Kelele za chura hazimzuwii ng'ombe kunywa maji.
139. Kelele za mlango haziniwasi usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba)
140. Kenda karibu na kumi.
141. Kesho kesho, kesho kiama.
142. Kiburi si maungwana.
143. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.
144. Kichango kuchangizana.
145. Kidole kimoja hakivunji chawa.
146. Kikulacho ki nguoni mwako.
147. Kikushindacho kukila usikitie ila.
148. Kila chombo kwa wimblile.
149. Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao.
150. Kila mlango na ufunguwo wake.
151. Kila mtoto na koja lake.
152. Kila mtu huzikwa na kaburi lake.
153. Kila mtu na bahati yake.
154. Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
155. Kila mtu hulilia mamae.
156. Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
157. Kila shetani na mbuyu wake.
158. Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
159. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
160. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
161. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
162. Kingiacho mjini si haramu.
163. Kinyozi hajinyoi.
164. Kinywa ni jumba la maneno.
165. Kipendacho moyo dawa.
166. Kipofu hasahau mkongojo wake.
167. Kipya kinyemi ingawa kidonda.
168. Kisebusebu na kiroho papo.
169. Kisokula mlimwengu, sera nale.
170. Kisokula mlimwengu,sera nale.
171. Kisu kimenifika mfupani.
172. Kitanda usicho kilalia hukijui kunguni wake.
173. Kitumbua kimeingia mchanga.
174. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
175. Kiwi cha yule ni chema cha; hata ulimwengu uwishe.
176. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
177. Konzi ya maji, haifumbatiki.
178. Konzo ya maji haifumbatiki.
179. Kosa moja haliachi mke.
180. Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
181. Kuagiza kufyekeza.
182. Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
183. Kucha M'ngu si kilemba cheupe.
184. Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi.
185. Kufa kufaana.
186. Kufa kwa jamaa, harusi.
187. Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
188. Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa.
189. Kuishi kwingi, kuona mengi.
190. Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
191. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
192. Kukopa harusi kulipa matanga.
193. Kukopa harusi, kulipa matanga.
194. Kuku havunji yai lake.
195. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
196. Kula kutamu ,kulima mavune.
197. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
198. Kukopa harusi, kulipa matanga.
199. Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.
200. Kunako matanga kume kufa mtu.
201. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
202. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
203. Kupata si werevu, na kukosa si ujinga.
204. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
205. Kurambaramba ndio kula, kunenepa kwake Mola.
206. Kusikia si kuona.
207. Kutangulia si kufika.
208. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
209. Kutu kuu ni la mgeni.
210. Kuugua sio kufa.
211. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
212. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
213. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
214. Kweli ilio chungu, si uongo ulio mtamu.
215. Kwenda mbio siyo kufika.
216. Kwenye miti hakuna wajenzi.
217. La kuvunda halina rubani.
218. La kuvunda halina ubani.
219. Lake mtu halimtapishi bali humchefua.
220. Leo kwako, kesho kwa mwenzio.
221. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
222. Liandikwalo ndiyo liwalo.
223. Lila na fila hazitangamani.
224. Lipitalo, hupishwa .
225. Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
226. Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
227. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
228. Maafuu hapatilizwi.
229. Macho hayana pazia.
230. Mafahali wawili hawakai zizi moja.
231. Maiti haulizwi sanda.
232. Maji hayapandi mlima.
233. Maji hufuata mkondo.
234. Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaoga.
235. Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
236. Maji ya kifuu, bahari ya chungu.
237. Maji yakijaa hupwa.
238. Maji yakimwagika hayazoleki.
239. Maji yamenifika shingoni.
240. Majuto ni mjukuu.
241. Mali ya bahili huliwa na wadudu.
242. Mama ni mama, hata kama ni rikwama.
243. Mama nipe radhi kuishi na watu kazi.
244. Mambo kunga.
245. Manahodha wengi chombo huenda mrama.
246. Maneno makali hayavunji mfupa.
247. Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni.
248. Maneno si mkuki.
249. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
250. Masikini akipata matako hulia mbwata.
251. Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
252. Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.
253. Maskini hana kinyongo.
254. Mavi usioyala, wayawingiani kuku?
255. Mavi ya kale hayanuki.
256. Mbinu hufuata mwendo.
257. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
258. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
259. Mchagua jembe si mkulima.
260. Mchagua nazi hupata koroma.
261. Mchagua nazi si mfuaji.
262. Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
263. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
264. Mchamba kwingi mara ujitia dole.
265. Mcheka kilema hafi bila kumpata.
266. Mchele mmoja mapishi mengi.
267. Mchelea mwana kulia hulia yeye..
268. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
269. Mcheza kwao hutuzwa.
270. Mcheza na tope humrukia.
271. Mchezea mavi, hayaachi kumnuka.
272. Mchezea zuri, baya humfika.
273. Mchimba kisima hungia mwenyewe.
274. Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
275. Mchuma janga hula na wakwao.
276. Mchumia juani,hulia kivulini.
277. Mdharau biu, hubiuka yeye.
278. Mdharau mwiba humchoma.
279. Meno ya mbwa hayaumani.
280. Mfa maji haachi kutapatapa.
281. Mfa maji hukamata maji.
282. Mficha uchi hazai.
283. Mfinyazi hulia gaeni.
284. Mfuata nyuki hakosi asali.
285. Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
286. Mgaagaa na upwa hali ugari kande.
287. Mganga hajigangi.
288. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
289. Mgeni ni kuku mweupe.
290. Mgeni njoo mwenyeji apone.
291. Mgomba haushindwi na mkunguwe.
292. Mgonjwa haulizwi uji.
293. Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
294. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
295. Mjinga mpe kilemba utamuona mwendowe.
296. Mjumbe hauawi.
297. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
298. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
299. Mkamia maji hayanywi.
300. Mkamia maji hayanywi.
301. Mkataa la mkuu huvunjika guu.
302. Mkataa wengi ni mchawi.
303. Mkataa ya Musa hupata ya Firauna.
304. Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
305. Mkono moja hauchinji ng'ombe.
306. Mkono moja haulei mwana.
307. Mkono mtupu haulambwi.
308. Mkono usioweza kuukata,ubusu.
309. Mkosa kitoweo humangiria.
310. Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu.
311. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
312. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
313. Mla cha uchungu na tamu hakosi.
314. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea.
315. Mla mbuzi hulipa ngombe.
316. Mla mla leo mla jana kala nini?
317. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
318. Mlala na maiti haachi kulia lia.
319. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
320. Mlimbua nchi ni mwananchi.
321. Mnyamaa kadumbu.
322. Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu yake i pale pale.
323. Moja shika, si kumi nenda urudi.
324. Moto hauzai moto.
325. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
326. Mpanda ngazi hushuka.
327. Mpanda ovyo hula ovyo.
328. Mpemba akipata gogo hanyii chini.
329. Mpemba hakimbii mvua ndogo.
330. Mpende akupendae asiyekupenda achana naye.
331. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
332. Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
333. Msafiri kafiri.
334. Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
335. Msasi haogopi mwiba.
336. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.
337. Msema pweke hakosi.
338. Mshika kisu, hashiki makalini.
339. Mshale kwenda msituni haukupotea.
340. Mshoni hachagui nguo.
341. Msi bahati, habahatishi.
342. Msi mbele, hana nyuma.
343. Msishukuru mja, hamshukuru Molawe.
344. Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
345. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
346. Mstahimilivu hula mbivu.
347. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
348. Mtaka lake hasindwi.
349. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
350. Mtaka unda haneni.
351. Mtaka uzuri hudhurika.
352. Mtaka yote hukosa yote.
353. Mtegemea nundu haachi kunona.
354. mtegemea nundu, haachi konona.
355. Mtego bila ya chambo, haunasi.
356. Mtembezi hula miguu yake.
357. Mteuzi heshi tamaa.
358. Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
359. Mtondoo haufi maji.
360. Mtoto akililia wembe mpe.
361. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
362. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
363. Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
364. Mtu hujikuna ajipatapo.
365. Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani.
366. Mtumai cha ndugu hufa masikini.
367. Mtumi wa kunga haambiwi maana.
368. Mtumikie kafiri upate mradi wako.
369. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
370. Muhitaji khanithi walau kana rijaali.
371. Muiba yai leo kesho hua mwizi wa ng'ombe.
372. Mume wa mama ni baba.
373. Mungu hamfichi mnafiki.
374. Mungu si asumani.
375. Muonja asali haonji mara moja.
376. Muuza sanda, mauti kwake harusi.
377. Mvua nguo, huchutama.
378. Mvumbika changa hula mbovu.
379. Mvumbika pevu hula mbivu na mvumbika changa hula mbovu.
380. Mvungu mkeka.
381. Mvunja nchi ni mwananchi.
382. Mvuvi ajuwa pweza alipo.
383. Mwacha asili ni mtumwa.
384. Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
385. Mwamini Mungu si mtovu.
386. Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
387. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
388. Mwana simba ni simba.The child of lion is a lion.
389. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
390. Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka, zuka naye.
391. Mwanga mpe mtoto kulea.
392. Mwangaza mbili moja humponyoka.
393. Mwanzo kokochi mwisho nazi.
394. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
395. Mwanzo wa ngoma ni lele.
396. Mwapiza la nje hupata la ndani.
397. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
398. Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota.
399. Mwenda mbio hujikwa kidole.
400. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
401. Mwenda pole hajikwai.
402. Mwenda wazimu hapewi panga.
403. Mwenda wazimu hapoi, bali hupata nafuu.
404. Mwenye haja hwenda chooni.
405. Mwenye kelele hana neno.
406. Mwenye kovu usidhani kapowa.
407. Mwenye kubebwa hujikaza.
408. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
409. Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
410. Mwenye macho haambiwi tazama.
411. Mwenye mdomo hapotei.
412. Mwenye nguvu mpishe.
413. Mwenye njaa hana miko.
414. Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
415. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
416. Mwenye shoka hakosi kuni.
417. Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
418. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
419. Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
420. Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
421. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
422. Mwomba chumvi huombea chunguche.
423. Mwosha hadhuru maiti.
424. Mwosha huoshwa.
425. Mwosha husitiri maiti.
426. Mzaha,mzaha, mara hutumbuka usaha.
427. Mzazi haachi ujusi.
428. Mzigo usiouweza unaubebea nini?
429. Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
430. Mzika pembe ndiye mzua pembe.
431. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
432. Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.
433. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
434. Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
435. Nani kama mama?
436. Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona.
437. Nazi haishindani na jiwe.
438. Nazi mbovu harabu ya nzima.
439. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
440. Ndege mwigo hana mazowea.
441. Ndevu sio shani, hata beberu anazo.
442. Ndugu chungu, jirani mkungu.
443. Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
444. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
445. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
446. Ngoma ivumayo haidumu.
447. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
448. Ngoma ya kitoto, haikeshi.
449. Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
450. Ng'ombe haelemewi na nunduye.
451. Ngombe wa Maskini hazai.
452. Ngozi ivute ili maji. ( Udongo upate uli maji )
453. Nguo ya kuazima, Haistiri matako.
454. Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
455. Nifae na mvua nikufae na jua.
456. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
457. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
458. Nimerejesha kikombe na kisahani chake.
459. Njia ya muongo fupi.
460. Njia ya mwongo ni fupi.
461. Njia ya siku zote haina alama.
462. Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga.
463. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
464. Nyani haoni kundule.
465. Nyimbo mbaya haibembelezewi mtoto.
466. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
467. Nyongeza huenda kwenye chungu.
468. Nyota njema huonekana asubuhi.
469. Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
470. Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
471. Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. (Jihadi ya nzi, kufa kidondani)
472. Ondoa dari uwezeke paa.
473. Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
474. Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
475. Painamapo ndipo painukapo.
476. Paka akiondoka, panya hutawala.
477. Paka hakubali kulala chali.
478. Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya.
479. Paka wa nyumba haingwa.
480. Panapo wengi hapaharibiki neno.
481. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
482. Pele hupewa msi kucha.
483. Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
484. Penye kuku wengi usimwage mtama.
485. Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
486. Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.
487. Penye miti hakuna wajenzi.
488. Penye nia pana njia.
489. Penye urembo ndipo penye urimbo.
490. Penye wazee haliharibiki neno.
491. Penye wengi pana mengi.
492. Penye wengi pana Mungu.
493. Pilipili usoila, wewe inakuwashia nini?
494. Pole pole ndio mwendo.
495. Pwagu hupata pwaguzi.
496. Radhi ni bora kuliko mali .
497. Radhi za wazee, ni fimbo.
498. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
499. Sahau ni dawa ya Waja.
500. Samaki mmoja akioza, huoza wote.
501. Samaki mpinde angali mbichi.
502. Shida haina hodi.
503. Shida huzaa maarifa.
504. Shika! Shika! na mwenyewe uwe nyuma.
505. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
506. Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
507. Si kila king'aacho ni dhahabu.
508. Si kila mwenye makucha huwa simba.
509. Si Mungu mtupu na mkono wa mtu.
510. Sikio halilali na njaa.
511. Sikio halipwani kichwa. (Sikio halipiti kichwa).
512. Sikio Ia kufa halisikii dawa.
513. Siri ya mtungi aijuaye ni kata.
514. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia.
515. Siku njema huonekana asubuhi.
516. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
517. Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza.
518. Siku za mwizi, arubaini.
519. Simba mwenda kimya (pole) ndiye mla nyama.
520. Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
521. Sio shehe bali ni shehena.
522. Siri ya maiti aijuaye muosha.
523. Sitafuga ndwele na waganga tele.
524. Sitapiki nyongo harudi haramba.
525. Subira ni ufunguo Wa faraja.
526. Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu.
527. Sumu ya neno ni neno.
528. Tabia ni ngozi ya mwili.
529. Tamaa mbele, mauti nyuma.
530. Taratibu ndio mwendo.
531. Tawi kavu kuanguka si ajabu.
532. Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe
533. Tonga si tuwi
534. Tunda jema halikawii mtini.
535. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
536. Ujuzi hauzeeki.
537. Uchungu wa mwana, aujue mzazi.
538. Udongo uwahi ungali maji (Udongo upate uli maji)
539. Udugu wa nazi hukutania chunguni (Udugu wa nazi hukutana pakachani)
540. Uji hajauonja, tayari ushamuunguza
541. Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho.
542. Ukimpa shubiri huchukua pima.
543. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka Makalio.
544. Ukimwamsha alolala utalala weye.
545. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa.
546. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
547. Ukiona moshi, chini kuna moto.
548. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
549. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
550. Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma.
551. Ukistahi mke ndugu, huzai nae.
552. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
553. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona.
554. Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako.
555. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma.
556. Ukupigao ndio ukufunzao.
557. Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
558. Ulimi hauna mfupa.
559. Ulimi unauma kuliko meno.
560. Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
561. Ulivyoligema, utalinywa.
562. Umeadimika kama la jogoo.
563. Umegeuka mung'unye waharibika ukubwani.
564. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
565. Umekuwa bata akili kwa watoto?
566. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
567. Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
568. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
569. Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!!
570. Unakuja juu kama moto wa kifuu.
571. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
572. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
573. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie).
574. Usiache kunanua kwa kutega.
575. Usiache mbachao kwa msala upitao.
576. Usiache tawi kabla ya kushika tawi.
577. Usiandikie mate na wino ungalipo
578. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
579. Usijifanye kuku mweupe.
580. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno
581. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
582. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
583. Usiniache njia panda.
584. Usinikumbushe kilio matangani.
585. Usinipake mafuta kwa nyuma ya chupa.
586. Usinivishe kilemba cha ukoka.
587. Usione simba kapigwa na mvua.
588. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
589. Usisafirie nyota ya mwenzio.
590. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
591. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.
592. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
593. Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo.
594. Utakosa mtoto na maji ya moto.
595. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
596. Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua.
597. Vita havina macho.
598. Vita si lele mama.
599. Vita vya panzi, neema ya kunguru
600. Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba
601. Wache waseme.
602. Wafadhilaka wapundaka.
603. Wagombanao ndio wapatanao.
604. Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma.
605. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo ni nyasi.
606. Watetea ndizi, mgomba si wao.
607. Wazuri haweshi.
608. Wema hauozi..
609. Wengi wape.
610. Zinguo la mtukufu, ni ufito.

0 maoni:

BABA SHIKA USHIKAPO

Sikiliza shairi likiimbwa kwa sauti ya kipekee na mghani,shairi hili ni jibu kwa bwana Abeid.

0 maoni:

UHUSIANO WA FASIHI NA JAMII KATIKA MITIZAMO YA FASILI ZA FASIHI

UHUSIANO WA FASIHI NA JAMII WAWEZA KUTAZAMWA KWA FASULI YA MITAZAMO IFASILIYO FASIHI

na
ALCHERAUS R. MUSHUMBWA
Mwl, Shule ya Upili Mwang’halanga
Kwimba, Mwanza – Tanzania

       Ikisiri
Fasihi na Jamii ni dhana ambayo imekuwa ikishughulikiwa sana na kwa kina miongoni mwa wanafasihi pamoja na wahakiki wa fasihi. Aidha, kulingana na upeo pamoja na mlango wa kiutafiti wa mtaalamu, dhana hizi zimekuwa zikifasiliwa na kufafanuliwa kwa mielekeo kulingana na mtaalamu husika; zaidi zimekuwa zikifafanuliwa ama kama dhana mbili tofauti ila zenye kujengana; au,  kama dhana moja inayounganishwa kwa dhima. Kutokana na dhana hizi kuwa na umuhimu mkubwa katika taaluma ya fasihi, makala haya yanalenga si kuleta jambo jipya; bali, kuendeleza utamaduni wa kufafanua dhana hizi kwa mlengo tofauti kidogo.
        Kama mada inavyosomeka, makala haya yanajaribu kufafanua uhusiano wa fasihi na jamii kwa mwongozo wa fasili za mitazamo inayotumiwa na wananadharia wa fasihi kufasili dhana ya fasihi. Katika kutimiza azma hiyo, makala haya yameteua mitazamo mikuu mitano ambayo kwayo fasili zake zinaigemeza fasihi moja kwa moja na jamii
Utangulizi
Fasihi kama tunda la juhudi za wanadamu, ambapo tunda hilo hukidhi kiu na hamu ya wanajamii wenyewe, basi haiwezi kwa hakika, kuachwa ikisimama yenyewe bila kuangaliwa chimbuko lake ambalo ni wanadamu. Kama fasihi chimbuko lake ni wanadamu basi wanadamu hao nao wana chimbuko lao nalo ni jamii waishimo. Vivyo hivyo, haiwezi kuhusishwa fasihi na wanadamu bila kuihusisha na jamii kwani jamii ndiyo chimbuko la wanadamu na ndilo vilevile, chimbuko la fasihi. Kwa maana hiyo basi, kuna unasaba wa wazi katika fasihi na jamii. Katika kudhihirisha hilo kwa ufupi, makala haya yanangazia baadhi ya mitazamo ya fasihi iliyoibuliwa na wanafasihi jinsi inavyoweza kusaidia kufasili uhusiano uliopo baina ya dhana za “Fasihi”’ na “Jamii.”  


      1.1 Maana ya Fasihi
Fasihi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali waliojikita kuichunguza, kwa kutaja baadhi yao. Wamitila (2008:13), anaifasili fasihi kuwa ni sanaa inayotumia lugha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na huathiri, hugusa au huacha athari fulani na hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii fulani. Simiyu (2011:9), anatoa maana ya fasihi kuwa ni sanaa inayotumia lugha na matendo kuwasilisha ujumbe juu ya maisha ya binadamu. Anahitimisha fasili yake kwa kusema kuwa fasihi hutumia lugha na matendo kama malighafi yake kupitisha ujumbe. Naye, Malenya (2012:40) anasema kwamba fasihi ni sanaa maalum ya matumizi ya lugha inayotoa mafunzo ambayo yanatumiwa kuielekeza jamii.
Katika fasili hizi za wanazuoni zilizorejelewa kwa ufupi; ni kwamba, tunaona kuwa wanasisitiza suala la sanaa (ufundi) kama sifa au kitambulisho cha fasihi.  Pia, wanatuonesha kuwa sanaa hiyo lazima itumie lugha ili kuweza kufikisha kile ilichokibeba. Lakini sanaa hiyo inakuwa na ujumbe (maudhui) ambayo kwayo ndiyo msingi mkubwa. Ujumbe huu ni maalumu kwa ajili ya jamii. Kwa mwongozo huu, tunaweza kuhitimisha kwa kauli moja kuwa, fasihi ni sanaa idhihirikayo kupitia lugha na matendo ya binadamu hasa pale inapotumika kwa dumuni la kufikisha maudhui yake kwa walengwa (hadhira) wanaoishi katika jamii fulani. Tunaposema fasihi tuna maana ya sanaa. Tunaposema sanaa tunalenga picha ya ufundi wa kuwasilisha lengo fulani. Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha hisia na mawazo ya binadamu kwa maandishi, michoro na uchoraji au uchongaji. Ama sanaa ni zao linalotokana na ufundi huo. Kwa hiyo, ufundi huo ndio tunaoita sanaa, na fasihi ni sanaa kwa sababu huwasilisha mafunzo yake kwa kutumia ufundi huo unaojipambanua kwa mbinu ya lugha ya binadamu.
        1.2 Dhana ya Jamii
Jamii ni msamiati ambao katika maisha ya kila siku tunautumia kuashiria maana fulani; ama, kulingana na muktadha au kwa maana halisi ya kileksia. Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya (2004) inafafanua kiduchu maana ya neno “Jamii” kuwa ni mkusanyiko wa watu au vitu. Vilevile, Kamusi ya Kiingereza Oxford Advanced Learner’s Dictionary (2010), inafafanua kuwa Jamii ni watu kwa pamoja, waishio pamoja kwenye ujima; ni ujima fulani wa watu wenye desturi, tabia na sheria za aina moja. Simiyu (2011:20) anasema kuwa Jamii ni kikundi cha watu wanaotumia lugha moja, wana utamaduni mmoja na wanapatikana katika eneo moja la mastakimu. Kwa hiyo, kwa maoni yetu, ni sawa kabisa kufasili Jamii kama mkusanyiko au kundi la watu waliokusanyika sehemu fulani kama kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda na taifa. Watu hawa huishi kama wamoja, na wenye kufuata utaratibu au kanuni fulani za kimaisha walizojiwekea wao wenyewe. Mkusanyiko huo wa watu unakuwa na utamaduni wake, unaodhihirika katika mila na desturi na mielekeo fulani ya kimaisha.

 “Fasihi na Jamii” kma dhana kuu
Baada ya kupata dondoo fupi kiasi juu ya dhana ‘Fasihi’ na ‘Jamii’ kila moja kivyake, ni vema kuangalia pia juu ya dhana hizi mbili kama dhana moja.
 Madhali, fasihi ni sanaa ya lugha yenye kufikisha ujumbe kwa hadhira: basi wapokeaji wake ni watu ambao ni zao la jamii. Watu ni zao la jamii kwa kuwa jamii ndani yake kuna watu ambao hao huunda jamii. Basi tunaposema fasihi inatumia lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira (watu), moja kwa moja tunalenga kuwa fasihi inafikisha maudhui yake kwa wanajamii. Maoni haya ni sahihi kwa msingi wa kuwa ‘fasihi ni jamii na jamii ni fasihi’. Pengine, kauli ya kwamba fasihi ni jamii na jamii ni fasihi yaweza kukanganya kidogo miongoni mwa watu wanaoweza kusikia kauli hii. Ieleweke hakika, tusemapo kuwa fasihi ni jamii na jamii ni fasihi, ina maana ya kwamba bila jamii fasihi haiwezi kuwepo – kwamba, maisha ya fasihi yanategemea uwepo wa jamii. Na kwa maneno mengine ni kuwa, maisha ya jamii ndiyo chanzo cha fasihi. Vilevile ni wazi kuwa jamii ni fasihi kwani hakuna jamii inayoweza kuwepo bila fasihi. Fasihi ni sehemu ya na ni maisha ya jamii husika. Kwa mwelekeo huu, ni wazi ya kuwa wanajamii ndio wanafasihi; na wanafasihi ndio washughulikao na fasihi au kuidhihirisha na kisha kuitumia sanaa hiyo kueleza bayani jamii yao. Katika kuielezea jamii, fasihi hushughulikia kuonesha mambo yote yaliyomo katika jamii na kuifanya jamii itambulike na kuheshimiwa. Hivyo, fasihi na jamii ni kama pande mbili za sarafu moja.  Kutokana na maelezo haya, ndio sababu makala hii imeteua baadhi ya mitazamo inayoweza kudhihirisha uhusiano uliopo baina ya fasihi na jamii. Uhusiano huo ndio msingi wa makala haya kuwa “fasihi na jamii” mbili zinazojenga kitu kimoja nza zikishaungana na kutengeneza kitu kimoja ni vigumu kuzitenganisha. Baadhi ya mitazamo hiyo inayojadiliwa hapa ni: Fasihi ni Hisi, Fasihi ni Kioo cha Jamii, Fasihi ni Mwavuli wa Jamii, na Fasihi ni Zao la Jamii husika na Mielekeo yake ya maisha.
Mitazamo inayofafanua Uhusiano wa Fasihi na Jamii
Kama lilivyo lengo la makala haya kwamba mchango wake ni kuongeza mchango katika kufafanua uhusiano uliopo baina ya fasihi na jamii. Kipengele hili kinajadili kwa kiwango fulani jinsi baadhi ya mitazamo ya kuifasili fasihi iliyoteuliwa kwenye makala haya inavyodokeza bayani uhusiano kati ya fasihi na jamii. Imeteuliwa mitazamo mikuu mitano ambayo kinaganaga ufafanuzi wake unadhihirisha uhusiano wa ndani na nje wa fasihi na jamii.
Fasihi ni Hisi zipatazo Taarifa kuoka katika Jamii
Fasihi imekuwa ikielezwa katika mtazamo wa hisi. Baadhi ya wanazuoni wamedhubutu hata kukosoa kuwa si vema kuiona fasihi ni hisi, hasa wakiegemea zaidi katika fasili ya hisia za kuguswa moyoni. Kwamba, fasihi ni hisia zitokanazo na mguso wa ndani wa moyoni mwa binadamu au mwanafasihi (msanii). Wanaochukulia mtazamo huu katika mawazo hayo, wanakwenda kinyume kabisa na mtazamo huu kwa kusema kwamba si vema kusema kuwa fasihii ni hisi kwa mwelekeo wa mawazo ya kuwa msanii anaamua kufikisha maudhui yake kwa wapokeaji wake baada ya kuguswa na baadhi ya mambo mbalimbali katika jamii. Na hivyo, kutoa maoni kuwa anapoguswa msanii ndipo anapokuja na jambo na kulieleza kwa maandishi au kwa nyimbo, hadithi, na kucheza. Wanaendelea kwenda kinyume kwa kuhoji kwa hoja kwamba kama fasihi ni mguso au hisia za msanii; je inakuwaje baadhi ya wasanii wanaotoa kazi zao za fasihi zaidi ya moja, wanakuwa wameguswa mara ngapi? Mfano; waandishi wa zamani wa fasihi ambao hawapo tena duniani, wameguswa hadi hivi leo? Ukizingatia kazi zao hadi hivi sasa zinafanya vizuri katika jamii. Hayo ndiyo mawazo kinzani juu ya mtazamo wa “fasihi ni hisi.”
      Lakini kwa tafakuri yetu, tunabainisha upungufu wa upande ulioelezwa mwanzo juu ya maoni ya wanaopinga dhana ya kuwa fasihi ni hisi. Kwani, ukosoaji wao unaonekana ni matokeo ya kutowaelewa vizuri washadadizi wa mtazamo huu. Inaonekana sio sahihi kuiangalia fasihi kama hisia-mguso (wanaokosa mtazamo huo wanaiona fasihi kama hisia mguso). Bali, mtazamo huu wa “Fasihi ni Hisi” utazamwe sahihi, na kuutazama sahihi ni kuutazama katika uelewa wa hisi za mwili wa binadamu. Yaani, hisi tano za mwili wa binadamu (macho, pua, ngozi, masikio na ulimi) ndizo nyenzo kuu zimpatiazo msanii taarifa au ufahamu. Kwa sababu hisi hizi humpatia taarifa mwanafasihi/fanani, mtu huyo hufikisha ujumbe wake kwa wapokezi kwa daraja murua ambalo ni lugha. Sengo na Kiango ni wadau wakubwa katika kuupa heko mtazamo huu; wanasema wazi kuwa:
Ikiwa tutasema fasihi ni hisi ni sawa, lakini jibu lenyewe halitoshelezi haja za kazi, athari na thamani ya neno lenyewe na kitu chenyewe kwa jamii. Mtu asikiapo njaa, ama aonapo baridi, si kwamba anatumia macho kwa kuona baridi bali anatumia ‘hisi’ kwa kuchokonoa utashi wa yote ya mawili. Swali: Je hisi hii ni fasihi? Kwa nini isiwe kama fasihi ni hisi? Kwa upande inaweza ikasemekana kwamba hisi ya njaa, baridi, uchovu n.k. ni sawa na ile ya fasihi kuwa vifaa vinavyotumika kuielezea hali ya hisi hizi zote ni vimoja; kwamba mtu hutumia hisi tano za mwili kujiona kwamba yu mwitaji wa chakula. Lugha, ama ishara nyingine ya aina yake inatumika katika kulieleza tatizo la mhusika. Katika ‘fasihi’ pia, hisi tano za mwili hutumika na lugha ndio kielelezo cha matokeo ya hisi hizo (1973:3).
Hivyo basi, ni dhahiri kwamba mtazamo wa Sengo na Kiango unatupa picha halali kuhusu mtazamo unaosema “fasihi ni hisi”, kwamba binadamu hutumia hisi tano kupata taarifa kutoka kwenye jamii yake na kutumia sanaa ya fasihi kuwasilisha taarifa hizo kwa jamii pia. Taarifa hizo zaweza kuwa mbaya, nzuri; ama za kuonya, kutaarifu, kuliwaza, kuelimisha, mtawalia. Jambo tunaloweza kulieleza hapa ni kwamba mtazamo huu uko sahihi na unaleta mantiki, kwani kwa wigo mpana unatupa taswira mwafaka ya ndoa iliopo kati ya fasihi na jamii. Hivi kwamba, unatuonesha kuwa kabla ya kukiwasilisha kwa hadhira kile kinachotakiwa kuwasilishwa kuna kitu kinachokiibua au kukibaini ambacho ni hisi. Hisi hizi zinatupatia taarifa kutoka katika jamii zetu tunamoishi na fasihi inatusaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikishia wanajamii taarifa hizo kwa ufasaha, na hata watu wa jamii nyinginezo vilevile. Kwa hiyo, ni wazi kuwa fasihi ambayo ni sanaa isingekuwepo kama binadamu asingeumbwa na milango ya fahamu ambayo kwa mtazamo huu ni hisi zinazompatia msanii taarifa anazoziwasilisha kwa njia ya fasihi. Mtazamo huu unaweza kuthibitishwa vizuri na msanii wa sinema za kitanzania, Steven Kanumba katika sinema yake inayoitwa Moses ambapo mhusika mkuu anaonesha jinsi hisi zake za ufahamu zilivyoshuhudia mambo katika maisha yake yaliyomfanya atunge kazi hiyo.
Fasihi ni Kioo cha Jamii
Fasihi kama ufundi na mbinu mwafaka za kufikisha ujumbe kwa hadhira; imefananishwa kama kioo cha jamii husika. Katika mtazamo huu, fasihi inakuwa kioo cha jamii kwani inaaksi matendo ya jamii na kuyaonesha kwa umma. Katika kutimiza azma hii, fasihi inapoaksi jamii yoyote ile, wanajamii wanajiona kupitia kioo hicho. Baada ya kuona taswira zao kwenye kioo, watu wanaona mapungufu yao na kuyarekebisha. Hili linaendana sambamba na jamii kujifunza, kuburudika, kuonywa, na kujirekebisha. Kwa sababu jamii inajiona yenyewe katika kioo (fasihi) kupitia taswira iliyoaksiwa; hivyo, jamii inajierkebisha. Kwa kuwa mtu anapotazama kioo huona taswira yake, na baada ya kugundua sura yake hajaiweka sawa, mtu huyo hujirekebisha ili awe sawa sawia. Maneno haya yanaungwa mkono na wataalamu kama Masebo na Nyangwine (2007:1), pale wanaposema kuwa “mtu anaweza akajitazama akaona taswira yake na akajirekebisha.” Vivyo hivyo, jamii husika inaweza kujifahamu kupitia fasihi yake na kujirekebisha.
Mtazamo huu umejaribiwa kukosolewa na baadhi ya waandishi na watafiti wa fasihi. Miongoni mwa wakosoaji ni Lubandanja na wenzake (2016:3) ambapo wanahoji kwamba “kuchukulia fasihi kama kioo siyo sawa kwani kioo hakiwezi kuonyesha sehemu (sura) zote za mwili ama kitu. Je, fasihi haiwezi kuonyesha maisha yote ya jamii?”
      Kama walivyohoji Lubandanja na wenzie juu ya udhaifu wa mtazamo huu, ukweli ni kwamba swali lao linajijibu lenyewe kwani, kama ilivyo kioo kutoweza kuonesha sehemu zote za mwili wa biadamu bali sehemu tu ya sura yake ndivyo ilivyo pia kwa fasihi kuwa haiwezi kamwe kuangazia maisha yote ya jamii bali huangazia baadhi ya mambo ya kimaisha ya jamii husika kulingana na wakati na lengo la msanii. Endapo tutakubali kuwa fasihi inaangazia maisha yote ya jamii kwa pamoja: (i) ni kuidunisha na kuidumaza jamii kuwa haibadiliki na haiendani na mpito wa wakati. Jamii hudumu milele ila katika mabadiliko yanaoyobainishwa na vipindi mbalimbali na mpito wa kimaisha, na mbadiliko haya huibua mifumo mbalimbali ambayo jamii husika hupitia na mifumo hiyo, kila mfumo huibuka na mtindo fulani wa fasihi unaoeleza jamii hiyo katika mfumo iliyomo. (ii) ni sawa na kusema kuwa hakuna haja ya kuendelea kutunga kazi za fasihi kwani zile zilizokwishatungwa zinatosha na kwa kuwa fasihi huangazia maisha yote basi kazi ambazo zimeshatungwa ziliangazia kila kitu katika jamii zetu na hivyo haina haja tena ya wasanii wapya kutunga kazi mpya za fasihi; (iii) kila kazi ya fasihi hushugulikia masuala kadhaa ya kijamii, ambayo kulingana na uwezo na ufahamu wa mtunzi unapofikia juu ya kuyang’amua mambo ya kijamii. Kwa hiyo, ni vigumu fasihi kuangazia mambo yote ya kimaisha ya jamii husika kwa wakati mmoja na kuyamaliza.
     Mbali na hayo, vyovyote iwavyo, mtazamo wa kuifasili fasihi kama kioo cha jamii, ambacho wanajamii husika hujitazama na kujirekebisha kwa yale yasiyofaa na kudumisha yale mazuri, unatupa mwanga wa kuona kuwa jamii inatumia fasihi kama chombo kujitazama na kujikosoa, kujifunza na kuhimarisha yale yaliyo bora. Mathalani kazi za fasihi karibia zote hufanya kazi ya kioo kama ilivyotajwa, miongoni mwa kazi zinazothibitisha ukweli huo ni kama tamthiliya za Kaptula la Marx (1996) yake E. Kezilahabi na Nguzo Mama (1982) ya P. Mhando. Katika kazi ya Kaptula la Marx inaoneshwa jinsi jamii wa wakati huo ilivyokuwa imekengeuka kwa uongozi wa kiongozi waliyekuwa na imani naye tena imani kuu ya aina ya uongozi wake jambo ambalo linasababisha hali ya jamii hiyo katika nyanja zote za jamii kimaendeleo kupwaya kwa sababu ya mfumo wa utwala uliokuwepo jambo ambalo baadae jamii hiyo ilikuja kubadilika na kubadilisha aina ya uongozi wake kutoka katika ujamaa hadi mfumo wa sasa wa demokrasi na soko huria. Kaprula la Mar ni kazi inayokejeli utawala huo. Vilevile, katika tamthiliya ya Nguzo mama msanii anatumia kazi hiyo kuionesha jamii ilivyo na utamaduni mbovu wa kuwakandamiza wanawake na kupendekeza juhudi za ukombozi wa wanawake jambo ambalo kwa sasa limeshika mizizi na jamii zinabadilika. Hivyo, kazi hizi zimetumika kama vioo vya kuaksi uhalisia wa maisha ya jamii na jamii kuchukua hatua za kujirekebisha.
Fasihi ni Mwavuli wa Jamii
Mwavuli ni kifaa kitumikacho kumkinga binadamu dhidi ya jua na mvua. Kumkinga huko ni kumlinda mtu dhidi ya adha za jua na mvua; na kitendo hiki tunaweza kukiita “kutunza/utunzaji”. Aidha, fasihi nayo tunailinganisha na mwavuli, kwani inatekeleza jukumu kama lile la mwavuli. Fasihi na jamii ni mambo yasiyoweza kutenganishwa. Fasihi yoyote ile, iwe ya masimulizi au ya maadishi, inalinda, inakinga na kuitunza jamii. Kwa kuliona hilo kuwa ni jukumu kuu la kazi ya fasihi iwayo yoyote ile, Sengo na Kiango kwa wasaa mwingine wanajitokeza na kusema:
Fasihi ni kama mwavuli umkingao mtu na mvua au jua; mwavuli-fasihi ni ule uhifadhio amali za maisha ya watu wote bila kuchagua wala kubagua tofauti zilizopo.  [. . .] Amali hizo ndizo zijengazo fasihi. Baada ya kujengwa na jamii, fasihi inazihifadhi. Huzifichua na kuzionyesha amali hizo kwa watu ili waone ubora na uovu wa kila kipengele cha maisha kwa mbalimbali: kwa kujadili, kushauri, kuasa, kuusia, kuadibu, kuelimisha (1973: 3).
        Fasihi inauvaa uhusika wa mwavuli kutokana na kuikinga au kuilinda jamii hasa pale inapozihifadhi amali za jamii ili zisiharibiwe na muda mwingine inazionesha wazi kwa watu na kubaini zile zilizo bora na zile zilizopitwa na wakati. Kulingana na mabadiliko ya wakati amali zisizofaa au kupitwa na nyakati zinaachwa na kutupiliwa mbali; pia fasihi inazihifadhi kama kumbukumbu ili vizazi vinavofuata vijifunze na kuchukua tahadhari. Kwa maana hiyo, kutokana na fasihi kuwa kama mwavuli, tunapata kujua mila na desturi nzuri ambazo kabla ya uwepo wetu zilikuwa zikiishi na zile ambazo ni mbaya zilizofanywa na baadhi ya wanajamii na hivyo kutuwezesha kuendelea kudumisha zile mila nzuri na kutupilia mbali na kupiga vita zile mila mbovu. Kutokana na fasihi kubeba jukumu kama la mwavuli la kuikinga na kuilinda jamii dhidhi ya uovu, wanajamii huwa na tahadhari ya kutokufanya mambo mabaya ambavyo ni kinyume na utamaduni wao ili kulinda heshima na utu wa jamii zao. Tuchukulie mfano wa sinema ya The Devil Kingdomambayo maudhui yake ni kuonesha jinsi watu wanavyotumia mbinu zisizofaa za ushirikina ili kujipatia mali na mwisho wa siku wanajikuta wamefanya makosa ya kumhasi Mungu wao na kuamua kumrudia kwa kutubu na kurudi katika hali ya uchaji Mungu. Mfano mwingine ni mfano wa mashairi ya “Uungwana Kitu Mbali na Vita Havitakuvusha” kutoka katika Diwani ya Midulu. Mashairi haya kwa hakika yanaonesha kutetea mila, desturi na utaratibu wa waungwana wa kutetea uungwana na utulivu au ulindaji wa amani ambayo ni mambo mazuri na amali za jamii ya msanii mtunzi wa kazi hizo. Hivyo maudhui yake ni kukemea watu wanaofanya maovu kwa kukiuka mila na desturi pamoja na wale wanaopenda uvunjifu wa amani kwa kuona kuwa vita ndio njia ya kujenga amani.
 Fasihi ni zao la Jamii na Mielekeo yake
Fasihi ni zao la jamii kwa sababu inatokana na jamii, hivi kwamba wanafasihi ni wanajamii wa jamii fulani na yale wayawasilishayo kwa kutumia fasihi chanzo chake ni jamii na huwafikia jamii pia. Pamoja na kuwa ni zao la jamii fulani, fasihi ni lazima iwe au ifuate mwelekeo fulani wa jamii. Fasihi inajidhihirisha kama zao la jamii kwani, fasihi yoyote ile lazima itolewe na jamii au watu wa jamii hiyo. Kwa hiyo, bila jamii hakuna fasihi. Fasihi kama sanaa, na sanaa hiyo imo ndani ya jamii kwa kupitia mahuluti ya msanii anavyopenda kuufikisha ujumbe kwa hadhira yake ambayo ni jamii. Sambamba, fasihi huendana na mielekeo fulanifulani ya kimaisha katika jamii kwa jinsi ambavyo inatakiwa. Ni ndani ya jamii, fasihi haivuki. Na kwa maana hiyo fasihii lazima iwe na mipaka kuhusu maisha ya jamii inapohusika. Mila na desturi za jamii zinaelezwa na fasihi husika. Fasihi humfanya mtu mwingine aijue jamii fulani kwa kupitia fasihi yake. Fasihi inaweza kutazamwa kama kiwakilishi cha jamii inayohusika. Kwa mfano, katika nchi za eneno la Afrika Mashariki kuna jamii ambazo miongoni mwa uatamaduni wao ni kufanya matukio ya kuwakuza vijana – yaani kuonesha kuwa kijana ametoka katika hatua ya utoto sasa kawa kijana na mtu mzima maarufu kama ‘Jando na Unyago.’ Matukio haya hufanywa kwa kuambatanishwa na fasihi inayoelezea utamaduni huo hasa nyimbo za jando na unyago au tohara. Pia, kuna nyimbo za dini za kuabudu na kusifu. Kazi ijulikanayo kama Utu bora Mkulima (1969) ya S. Robert ni mfano wa fasihi inayoonesha kuwa ni matokeo ya jamii ya wakati huo na mielekeo yake chini ya falsafa ya ujamaa na kujitegemea ambapo watu walijengwa kwa msingi wa kilimo vijini. Hizi kazi zote za kifasihi ni fasihi inayotokana na jamii pamoja na kudokeza mielekeo ya jamii hizo. Kwa hiyo, mtu akiifahamu fasihi ya kabila fulani, basi mtu huyu analifahamu kabila kwa kiasi fulani. Atakuwa anajua sera, siasa, utendakazi, desturi na mila za kabila hilo ambapo mambo hayo yote ni mtokeo ya mielekeo ya jamii husika.
 Fasihi ni Kielelezo cha Jamii
Fasihi ni sanaa itumiayo lugha kufikisha maudhui kwa hadhira. Hadhira ndio walengwa wakuu wa kazi yoyote ya fasihi. Hadhira hao huwa ni wanajamii wa jamii fulani na msanii wa kazi ya fasihi naye pia ni mwanajamii wa jamii fulani. Hivyo, msanii huona, husikia, hufikiri na kutafakari kwa kina juu ya mambo katika maisha ya jamii husika. Akisha kuyabaini na kutafakari baadhi ya mambo katika jamii yake au hata jamii nyingine, msanii huyo, huamua kuyabeba katika umbo la sanaa na kisha kuyawasilisha kwa wanajamii wengine ili wapate kuyaona, kuyafikiria, kuyatafakari na kufahamu kipi kinachoendelea. Yale yote yanayokuwa yamebebwa katika kazi ya fasihi; si mengine, bali ni uwakilisho wa sehemu ya uhalisia wa maisha ya jamii hiyo kama: utamaduni – mila na desturi za jamii husika. Pia, kazi hiyo ya fasihi hujaribu kuonesha baadhi ya kaida na miongozo ya kimaisha ya jamii hiyo. Hivyo, katika kutimiza hayo, fasihi inakuwa inakamilisha jumuku la kuwa kielelezo cha jamii husika. Inakuwa ni kielezo cha kijamii kwa kuwa fasihi inawakilisha sehemu ya maisha ya jamii husika na kuwaonesha wengine kuijua jamii hiyo kupitia kazi fulani ya kifasihi. Fasihi, katika hilo inakuwa ni ishara fulani ya kuielezea na kuifasili jamii husika.
       Wataalamu wa fasihi, Wellek na Warren (1949) wakikubaliana na maoni ya De Bonald, wanaiona fasihi kama kielelezo cha jamii. Wanaamba kuwa “uhusiano kati ya fasihi na jamii hujadiliwa kwa kuanza na kauli ya De Bonald kwamba ‘fasihi ni kielelezo cha jamii.’”Aidha, kutokana ukweli huu tunweza kusema kwamba kazi nyingi za fasihi huwa ni vielelezo anuai vya jamii zao kwani hubeba na kuwakilisha sura za jamii hizo. Ipo mifano mingi ya kazi za kifasihi ambazo huwakilisha maisha ya jamii. Senkoro (1987) anadokeza wazi kuwa maendeleo pamoja na vpindi na mifumo mbalimbali amabayo jamii fulani hupitia huelezwa katika kazi mbalimbali za kifasihi. Hivyo, twaweza kusema maisha ya jamii husika, huweza kuelezeka katika kazi ya fasihi ya jamii hiyo na hivyo tunasema bila shaka kuwa fasihi hizo huwa ni vielelezo kwa jamii zinamoibuka. Mathalani, tukichukulia kazi ya riwaya ya Msomi Aliyebinafsishwa (2012) ya N. Nyangwine ni kielelezo cha jamii ya sasa ya utandawazi hasa iliyojikita katika mfumo wa ubepari wa soko huria ambapo dhana ya maendeleo kwa nchi maskini inasadikika kuwa ya kweli kupitia ubinafsishaji ambapo viongozi wa nchi maskini huweka rehani maliasili za mataifa yao kwa mabepari kwa njia ya ubinafsishaji huku awakijinufaisha wao viongozi na wawekezaji-wabinafsishaji na kuwaacha umma ukiteseka kwa umasikini.
Hoja zinazothibitisha Uhusiano wa Fasihi na Jamii toka kwenye Mitazamo ya iliyoelezwa kudokeza Uhusiano huo
Imetanguliwa kuelezwa katika makala haya kuwa fasihi na jamii ni pande mbili za sarafu moja amabazo hukamilisha kitu kimoja chenye maana kamili. Aidha, dhana hii ndiyo inayotupa kiburi cha kueleza kuwa fasihi na jamii ni mambo yasiyoweza kutenganishwa kamwe na hii ni kwa sababu kuwa “fasihi (yoyote ile) huangaliwa kama asasi ya jamii (Simiyu, 2011:20).” Na kama fasili ni asasi ya kijamii basi haiwezi kutenganishwa na jamii na jamii nayo haiwezi kukana asasi yake. Mara baada ya kuona mitazamo minne iliyofafanuliwa vizuri jinsi inavyofasili dhana ya faihi na jamii, mitazamo hiyo inatupa uwezo wa kubaini hoja zinazothibitisha uhusiano uliopo kati ya fasihi na jamii na hivyo kuzifanya kuwa dhana moja. Zifuatazo ni sifa zinazodokeza uhusiano kati ya fasihi na jamii mara baada ya mitazamo tuliyodadavua:
     Kwanza, mwanafasihi au msanii wa fasihi ni zao la jamii. Tunaposema kuwa msanii wa fasihi ni zao la jamii ina maana kuwa msanii mwenyewe anatoka katika jamii na hivyo kama anatoka kwenye jamii basi ni mwanajamii. Na kama ni mwanajamii, kile anachokitunga hukipata kutoka katika jamii kwa kusaidiwa na milango yake ya ufahamu (hisi) na hukielezea kwa wanajamii wenzake ambao maudhui yanayokuwa yamebebwa na kazi yake ya kifasihi huwalenga na kuwahusu wanajamii wenzake. Kwa sababu hiyo basi tunashawishika kusema ya kuwa kwa kuwa fasihi hupatikana kutoka kwenye jamii na wahusika wote ni wana wa jamii basi maudhui yake huilenga jamii husika.
     Pili, kile anachotunga mwanafasihi hukitoa katika mazingira ya jamii fulani ambayo yeye ni mhusika kwa namna moja au nyingine. Kazi yake ya fasihi anayoiumba msanii, hutokana na ufahamu wa msanii mwenyewe juu ya maisha na matukio ya jamii hiyo kutokana na kufahamu miktadha anuai ya jamii hiyo. Maudhui huyaumba kulingana na aina ya mipaka ya muktadha wa jamii anayoitungia kazi hiyo ya fasihi. Kwa mfano, tukirejea kazi zilizotungwa zenye maudhui sambamba na yale ya kipindi cha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika zilikuwa zimeumbwa kwa kuzingatia mipaka ya jamii hizo pamoja na kuzungumzia mambo yaliyokuwa yakisumbua jamii hizo hasa suala la ukoloni. Mathalani kazi za Adam Shafi, Kasri ya Mwinyi Fuad (1975) na Vuta n’Kuvute (1999).
     Tatu, uwepo wa fasihi hudokeza na kuwakilisha matabaka yanayopatika katika jamii hiyo. Fasihi huongelea matabaka mbalimbali yanayopatikana kwenye jamii wanapoishi watu na wanajamii wenyewe ndio wamiliki wa matabaka hayo kama tajiri na masikini, wasomi na wasio wasomi, watawala na watawaliwa, watoto na watu wazima, wanawake na wanaume mtawalia. Matakaba hayo ndiyo hujenga jamii, na fasihi itungwayo kuhusu jamii fulani ni lazima idokeze moja wapo ya jozi ya matabaka yaliyotajwa. Msanii hutunga kazi yake ya fasihi akilenga kuwasilisha maudhui yanayogusa tabaka au matabaka fulani yenye mgongano. Kwa kudhihirisha hilo, tamthiliya ya Kinjekitile (1969) ya Hussein inawakilisha jamii ya watu wa tabaka tawaliwa linalopaza sauti zake na kupiga kelele juu ya unyonyaji na ukandamizwaji unaofanywa na tabaka tawala la wakoloni.
     Nne, fasihi ina sifa ya kuiga jamii. Yaani, msanii huiga mambo au matendo yanayofanywa na wanajamii wenzake na kuyawasilisha kwa wanajamii wenzake akionesha uzuri na ubaya wake. Aidha, wasanii wa maigizo na vichekesho huonesha baadhi ya tabia na matendo yanayofanywa na watu katika jamii zao. Kwa mfano, nchini Uganda kuna msanii mmojawapo wa vichekezo maarufu kama Teacher Mpamire (Mwalimu Mpamire) ambaye huwasilisha sanaa yake ya fasihi kwa mtindo wa maigizo kwa kuiga baadhi ya matendo na sifa za wanajamii wa jamii za Afrika Mashariki.
      Kwa kukomea hapa japo si mwisho wa yote, uhusiano wa fasihi na jamii unabainishwa na lugha inayotumika kuwasilisha kazi fulani ya fasihi kwa hadhira wa jamii. Sifa kuu ya fasihi inayoifanya itofautiane na sanaa nyinginezo ni matumizi ya lugha na lugha ni sifa imhusuyo binadamu na si wanyama. Binadamu ni wanajamii, na mwanafasihi ni mwanajamii pia; lugha aitumiayo binadamu huwa ni lugha ya jamii fulani. Kama lugha itumiwayo na binadamu ni lugha ya jamii fulani mwanafasihi naye ni binadamu na ni mwanajamii katika jamii fulani, basi bila shaka msanii huyo hutumia lugha ya jamii fulani kuumba na kuwailisha kazi yake ya kifasihi kwa hadhira wa jamii. Lugha inayotumiwa na jamii au binadamu hulenga kuwasiliana miongoni mwao na lengo kuu la kuwasiliana huwa ni kupata ujumbe maalumu. Kwa mantiki hiyo basi, lugha ya fasihi ni zao la jamii na hivyo, fasihi na jamii huhusiana kupitia lugha miongoni mwa sababu nyinginezo.
Dima ya Tanzu za Fasihi inavyodhihirisha uhusiano wa Fasihi na Jamii
 Fasihi inajitokeza kama sanaa ndani ya matawi yake makuu mawili; yaani, Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi. Matawi haya mawili ndiyo yanayokamilisha utendaji wa fasihi kwa jumla, kupitia tanzu za kila tawi. Aidha, nui mojawapo ya fasihi, ni Fasihi Simulizi. Hii ni fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo. Fasihi Simulizi inajitokeza kiutendaji kupitia matawi yake madogomadogo (tanzu) ambayo ni Semi, Ushairi, Maigizo na Hadithi. Kila kitawi kina kazi au dhima zake ambazo zinajitokeza kiutendaji zaidi katika jamii.  Fauka ya hayo, Fasihi Andishi ni fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi. Vivyo hivyo, nayo inadhihirisha utendaji wake kupitia tanzu zake ambazo ni Riwaya, Tamthiliya, Ushairi na Hadithi fupi. Tawi hili pia lina kazi zisizotofautiana na pacha wake (fasihi simulizi). Hivyo basi, kupitia Riwaya, Tamthiliya, Hadithi, Semi, Ushairi na Maigizo, fasihi hudhihirisha utendaji wake katika jamii husika. Kila kifani cha fasihi hutungwa kwa ajili ya jamii na huwasilishwa kwa njia ya lugha: ya mazungumzo au maandishi.
      Fasihi na jamii ni mambo ambavyo kuyatenganisha ni kuua mojawapo. Hii ni kwa kuwa mambo haya yanategemeana na kukamilishana. Bila fasihi, sio rahisi kuielewa jamii husika, na bila jamii sio rahisi kuilewa fasihi. Fasihi inatokana na watu waliomo katika jamii, pasipo na jamii hakuna watu. Kwa kuwa sanaa ya fasihi inatoka ndani ya wanajamii ambamo fasihi hiyo inachimbuka, ni mwelekeo sahihi wa mawazo kusema fasihi ina dhima katika jamii kwa jumla; kwa maana hiyo tunaangalia dhima za fasihi.  Fasihi ina dhima au kazi nyingi katika jamii ambazo wanajamii huzikubali na kuziishi. Dhima za fasihi katika makala haya zinatengwa katika mitizamo mikuu miwili ambayo ni Kuelimisha na Kuburudisha.
      Kwa kuanza na kueliemisha, fasihi inalo jukumu la kuwaelimisha wanajamii wake. Ili kukamilisha jukumu hili, fasihi inaonya, inarekebisha, inafahamisha, inatoa mawaidha nakadhalika. Aidha, fasihi uhifadhi amali za jamii. Jamii yoyote ile ina fasihi ambayo hushughulika na maisha ya jamii hiyo. Shughuli za kiutamaduni na mielekeo ya jamii. Mathalani, nyimbo za Jando na Unyago, tamthiliya ya ‘Kwenye ukingo wa Thim (1988)’. Hizi ni baadhi ya kazi za fasihi ambazo zinaeleza na kuenzi utamaduni wa jamii za Afrika Mashariki na kupitia kazi hizi na nyinginezo nyingi wanaafrika mashariki hujifunza mambo mengi juu ya maisha yao. Aghalabu, fasihi hukuza na kuendeleza lugha ya jamii pia. Hii ni moja wapo ya kazi za fasihi, kwani fasihi hutumia lugha ama maneno ya binadamu kufikisha maudhui katika wapokezi wake. Nyimbo za makabila zimechangia sana kukuza na kuongeza msamiati katika lugha ya Kiswahili, na lugha za makabila, mtawalia. Pengine maghani, nyimbo majigambo, mashairi, ngonjera, vichekesho, soga, methali, vitendawili, miviga nakadhalika; kwa pamoja vipera hivi vya fasihi vimechangia kwa kiasi kikubwa wanajamii kuelewa na kuzoea lugha yao.
      Kadhalika, fasihi inatoa mafunzo na maadili mbalimbali kwa kuonya, kusifu au kukashifu mambo katika jamii. Wimbo wa msanii Saida Karoli, ujulikanao kama ‘Kaisiki’, ni mfano bora unaodhihirisha kuonya, kukosoa, kukashifu na kukejeli baadhi ya mambo mabaya yanayotendwa katika jamii. Wimbo huu unawaonya vijana wa kike na wa kiume wanaoshirikiana na mabinti kutoa mimba. Pia, unakejeli na kukashifu kitendo cha watu kutuma watoto wa wengine, ilhali wao waliwakataa hata kutoa mimba zao. Mfano, baadhi mishororo katika wimbo huu inasema:
                                  Ubeti mmojawapo katika wimbo wa Saida Karoli: ‘KAISIKI’
Mhh…! Toina maani toina mwana, olaba wowaaaa?
Leba wazeea, omugongo gw’ainamileeee!
Owange otakutuma kaisiki iwe…. Owawe okanagagaaaa x2”
Owange otumile no’mubwankya…owange otumileeee,
Owange otumile no’mubwaigoro… owange otumileeee,
Owawe agirea Merisa, owaewe agireaaa?
Tafsiri:
Mhh…! Huna nguvu huna mtoto, utakuwa wa nani?
Ona umezeeka, mgongo umepinda!
Wa kwangu usitume we mama/msichana…wakwako umemtupa x2”
Wa kwangu umatuma hata asubuhi…wa kwangu unatuma,
Wa kwangu unatuma hata jioni…wa kwangu unatuma,
Wa kwako ameenda wapi Merisa, wa kwako ameenda wapi?
 Zaidi ya hayo, katika kutoa elimu, fasihi inaeneza na kuchochea ushirikiano katika jamii. Mfano mzuri ni tamthiliya ya Harusi (1993). Hii ni tamthiliya ambayo inahimiza na kueleza ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki (Kenya na Tanzania). Uhusiano huu si mwingine bali ni wa wanajamii.
      Mwendelezo wa kazi ya fasihi katika jamii unakomea katika dhima ya kutoa burudani kwa wanajamii. Fasihi ni sanaa itumiayo lugha iliyoumbwa kiufundi (fani) kufikisha ujumbe kwa hadhira. Katika fani, fasihi huwasilisha ujumbe kwa njia ya nyimbo, mashairi hadithi, maigizo na mbinu nyingine nyingi kulingana na matakwa ya mtunzi. Katika fani hii, jamii au wapokeaji wa fasihi huburudika pia kwa kufurahi sana, kucheka, na kuchangamsha bongo. Mathalani vitabu vya riwaya pendwa, kama za Erick Shigongo, hadithi za kimahaba, tamthiliya za kwenye runinga na vichekesho vinavyofanywa na wasanii kama vikundi vya “Orijino Komedi – TBC1, Ze Comedy – EATV na Futuhi – Star TV”. Hii ni badhi tu ya kazi za kifasihi zinazofanya kazi ya kuburudisha wanajamii wanaozipokea kazi hizo. Kimsingi dhana ya kuonesha dhima za fasihi katika jamii ni kudhihirisha unasaba uliopo baina ya fasihi na jamii kwa mantiki ya kwamba mitazamo inayoifasili fasihi na jamii ukweli wake unaoneshwa bayani na kazi za fasihi katika jamii.



Hitimisho
Kwa kuhitimisha inaweza kusemwa kuwa fasihi itazamwe kama kiwakilishi cha jamii inayohusikaambamo fasihi yenyewe imetokea. Hivyo, fasihi na jamii ni kitu kimoja - yaani ni sawa na sarafu inayokamilishwa na pande mbili au mtu ambaye anakamilika kwa mwili na roho vinapoungana. Kwa mantiki ya kuwa, pasipo jamii hakuna fasihi na hakuna jamii bila fasihi. Kila jamii lazima iwe na fasihi ambayo ndio kitambulisho chake. Dhana ya fasihi inajieleza maridadi hasa pale inapoangaliwa zaidi kwa kuihusisha na jamii. Jamii haiwezi abadani kujitenga na fasihi yake na fasihi haiwezi kuwa sanaa iliyokamilika kwa kujitenga na jamii; na kama itakuwa hivyo, hakika haitakuwa ni fasihi. Hii ni kwa sababu kwamba fasihi pamoja na kuwa ni miongoni mwa mazao ya jamii, pia ni “taasisi ya kijami; kwani tunaweza kusema kuwa kwani mara nyingi fasihi hutokana na uhusiano wa karibu sana na taasisi maalum za kijamii. Taasisi za kiuchumi, kisiasa, na kijamii zimekuwa na uhusiano mkubwa sana na utoaji wa fasihi na kila kazi ya fasihi kwa njia moja au nyengine, hudhihiri uweli huu (Ntarangwi, 2004: 21).”
Kama iliyodokezwa kwenye ikisiri, makala hii imechambu na kuchukua baadhi ya mitazamo ambayo kimsingi ufasili wake wa fasihi unaweza kusaidia kuifasili dhana ya uhusiano uliopo kati ya fasihi na jamii.

MAREJEO
Bukagile, G.R & Ngambeki, J. 2005. Kiswahili Kwa Shule za Sekondari. Dar es Salaam:
                  General Booksellers Ltd.
Hornby, A.S. 2010. Oxford Advanced Learners’s Dictionary. 8th Edition. New York: Oxford
             University Press.
Hussein, E. 1969. Kinjekitile. Nairobi: Oford University Press.
Hussein, E. 1988. Kwenye Ukingo wa Thim.Nairobi: Oford University Press.
Kanumba, S. 2011. Devil Kingdom (sinema). Dar es Salaam: The Great Films.
Kanumba, S. 2011. Moses (sinema). Dar es Salaam: The Great Films.
Karoli, S. 2000. ‘Kaisiki.’ Chambua kama karanga. Mwanza: Tivol Studio.
Kezilahabi, E. 1996. Kaptula la Marx. Dar es Salaam: Dar es salaam University Press.
Lubandanja, E.E.N, Robert, P & Sheltiely, D.D. 2016. Kito cha Fasihi: Kwa shule za Upili,
                  Vyuo vya kati na Ndaki. Geita: Lubandanjas’ Junior Publishers.
Malenya, M. M. 2012. Matumizi ya Lugha katika Fasihi Simulizi. Mwanza: Inland Press.
Masebo, J.A & Nyangwine, N. 2007.  Nadharia ya Fasihi. Dar es Salaam: Nyambari Nyangwine
               Publishers.
Muhando, P. 1982. Nguzo Mama. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Ntarangwi, M.2004. Uhakiki wa Kazi za Fsihi. Augustana College, Rock Island, IL 61201 Nyangwine, N.C.M 2012. Msomi Aliyebinafsishwa. Dar es Salaam: Nyambari Nyangwine
                   Publishers.
Robert, S. 1969. Utu bora Mkulima.Nairobi: Evans Brothers.
Sayari, A.J. 1993. Harusi. Dar es Salaam University Press.
Sengo T.S.Y & Kiango.D. 1973. Hisia Zetu Na1: Fasihi. Dar es Salaam: Institute of Swahili
                 Research University of Dar es Salaam.
Sengo, T.S.Y.M. 2015. Diwani ya Midulu. Toleo la pili. Dar es Salaam: AKADEMIYA
Senkoro, F.E.M.K. 1987. Fasihi na Jamii. Dar es Salaam: Press and Publicity Centre.
Shafi, A.S. 1999. Vuta n’Kuvute. Dar es salaam: Mkuki na Nyota Publishers.
Shafi, A. S.1975. Kasri ya Mwinyi Fuad. Dar es Salaam:
Simiyu, W F. 2011.  Kitovu cha Fasihi Simulizi. Mwanza: Serengeti Bookshop.
 Taasisi ya Ukuzajia Mitaala Tanzania, 1992. Kiswahili Vyuoni. Dar es Salaam: KIUTA.
TUKI, 2004.  Kamusi ya Kaiswahili Sanifu. Toleo la Pili. Kenya: Oxford University Press.
Wamitila, K. W. 2008. Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Publications.

0 maoni:

Copyright © 2012 JUKWAA LA KISWAHILI